Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bi. Pili Mnyema (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkoa wa Tanga, baada ya maafisa hao kufika ofisini kwake, kumuelezea juu ya ujio wao kutembelea vikundi vinavyojishughulisha na kilimo cha zao la mwani katika wilaya za Mkinga, Muheza na Pangani, ambavyo vimekubaliwa ombi lao la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). (06.06.2023)
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Janeth Rukanga akizungumza kwa nyakati tofauti na baadhi wanavikundi vya Zinduka, Shaurimoyo, Vumilia na Jitahidi vinavyojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga ambavyo vimefanikiwa kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ili kuongeza tija katika kilimo cha zao hilo katika Bahari ya Hindi. (06.06.2023)
Afisa Mfawidhi Ukuzaji Viumbe Maji TangaBw. Omary Mohamed akizungumza na baadhi ya wanavikundi vya Zinduka, Shaurimoyo, Vumilia na Jitahidi vinavyojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga ambavyo vimefanikiwa kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ambapo amewakumbusha namna ya kutumia vyema mkopo huo pindi watakapoupata ili kukuza kilimo cha zao la mwani na kuhakikisha wanazingatia masomo ya kilimo hicho. (06.06.2023)
Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Cassian Zacharia akizungumza na baadhi ya wanavikundi vya Zinduka, Shaurimoyo, Vumilia na Jitahidi vinavyojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga ambavyo vimefanikiwa kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ambapo amewaasa kuwa na umoja na kuhakikisha pindi watakapokuwa wakiuza zao la mwani wawe na sauti moja katika kupanga bei na kuondoa hali ya ubinafsi kwenye vikundi ili vikundi hivyo viwe imara na kunufaika na zao hilo. (06.06.2023)
Afisa Uvuvi Ukuzaji Viumbe Maji Tanga, Bw. Onesmo Mwanyumba akiwaelekeza baadhi ya wanavikundi vya Zinduka, Shaurimoyo, Vumilia na Jitahidi vinavyojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga ambavyo vimefanikiwa kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), namna ya ufungaji bora wa zao hilo ili lisiharibikeau au kukatika likiwa baharini (06.06.2023)
Picha ya pamoja ya wanavikundi vya Vumilia na Jitahidi vinavyojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, wakiwa na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkoa wa Tanga, baada ya kupatiwa mafunzo mafupi juu ya kilimo hicho na namna bora ya kuimarisha vikundi vyao wakati wakisubiri kukamilika kwa taratibu za kupatiwa mkopo usio na riba ambao waliomba kutoka serikalini na kukubaliwa ombi lao. Mkopo utatolewa kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). (06.06.2023)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni