Nav bar

Jumapili, 11 Juni 2023

MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA YAFANYIKA MKOANI MARA


 Afisa Uvuvi Mkuu, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bw. Fadhili Ruzika, akitoa mafunzo kuhusu Ufugaji samaki kwa njia ya Vizimba,  kwa wanavikundi wanaojishughulisha na ufugaji samaki ambao wanatarajiwa kupewa mikopo kwa ajili ya ufugaji samaki, katika Ukumbi wa Halmashauri ya Musoma Mkoa wa Mara, tarehe (06.06.2023)

Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Eliakim Mniko  akitoa mafunzo ya Ujasiliamali, Usimamizi wa Biashara na mikopo kwa vyama vya Ushirika ,vikundi,makampuni na watu binafsi (hawapo pichani) wanaojihusisha na Uvuvi katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara, ambao wanatarajia kupata mikopo ya vizimba na pembejeo zake  kutoka serikalini.(06.06.2023)

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Pudensiana Panga, akifafanua jambo kwenye mafunzo ya Ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Usharika, Vikundi na watu binafsi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Mkoa wa Mara.(06.06.2023)

Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, wa Manispaa ya Musoma, Bi. Asteria Ruzangi akiongea na wanufaika wa mikopo ya vizimba na pembejeo zake na kuwasihi watumie vizuri mikopo hiyo ili kiweza kuleta tija katika Manispaa hiyo, wakati wa mafunzo ya Ufugaji Samaki kwenye vizimba, Tarehe (06.06.2023)

Timu ya mafunzo ya Ufugaji Samaki kwa vizimba, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wanufaika wa mikopo nafuu ya Pembejeo ya Ufugaji Samaki wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Mkoa wa Mara.(06.06.2023)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni