Nav bar

Jumamosi, 1 Aprili 2023

ULEGA AINADI SEKTA YA UVUVI KIMATAIFA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb.),  ameshiriki na kutoa mada katika kikao cha kufunga Maadhimisho ya Mwaka wa Kimataifa wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Mdogo (International Year of Artisanal Fisheries and Aquaculture Duniani - IYAFA 2022).


Akitoa mada katika  maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Rome, nchini Italia Machi 31, 2023, Mhe. Ulega  alielezea kuhusu fursa iliyopo katika   kuendelea kuboresha mnyororo wa thamani wa uvuvi hususan zao la dagaa ambalo linavuliwa kwa wingi Nchini Tanzania ambalo linahusisha jamii kubwa ya wavuvi hususan wanawake.


Alitumia fursa hiyo pia, kuwaeleza Wadau wa Uvuvi katika Maadhimisho hayo kuwa katika mnyororo huo wa thamani wa uvuvi nchini Tanzania kuna uhitaji mkubwa wa kuwekeza katika uzalishaji wa chakula cha samaki kwa ajili ya Ukuzaji Viumbe Maji.


Katika hotuba yake kwa ulimwengu, Waziri Ulega alitoa rai ya kuendeleza usimamizi wa rasilimali ya uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ili Sekta ya Uvuvi Iendelee kuleta tija.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kilimo na Chakula (FAO), Dkt. QU Dongyu, alimshukuru Waziri Ulega kukubali mwaliko huo huku  akimuahidi kuwa Shirika lake litaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha Sekta ya Uvuvi.


Waziri Ulega alialikwa kushiriki katika maadhimisho hayo kutokana na Tanzania kufanya vizuri katika utekelezaji wa Mradi wa Uvuvi Mdogo (SSF GUIDELINES) ambapo ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuzindua Mpango kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza mwongozo wa uvuvi mdogo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb.), (kushoto) akipeana mkono na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kilimo na Chakula (FAO), Dkt. Qu Dongyu walipokutana katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Roma - Italia Machi 31, 2023. Pamoja na mambo mengine, Waziri Ulega alielezea uhitaji wa kuendelea kuboresha mnyororo wa thamani wa uvuvi hususan zao la dagaa ambalo linavuliwa kwa wingi Nchini Tanzania na kuhusisha jamii kubwa ya wavuvi hususan wanawake na  uhitaji Mkubwa wa kuwekeza katika uzalishaji wa chakula cha samaki kwa ajili ya Ukuzaji Viumbe Maji.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb.),  akitoa mada kwenye Mkutano wa kufunga Maadhimisho ya Mwaka wa Kimataifa wa Uvuvi Mdogo na Ukuzaji Viumbe Maji (IYAFA 2022) yaliyofanyika jijini Rome, nchini Italia Machi 31, 2023. Mhe. Ulega aliwakilisha bara la Afrika kutokana na Tanzania kuwa kinara wa utekelezaji wa Mwongozo wa Uvuvi Mdogo. Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kilimo na Chakula (FAO), Dkt. QU Dongyu.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb.), (kushoto) akizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kilimo na Chakula (FAO), Dkt. Qu Dongyu walipokutana katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Roma - Italia Machi 31, 2023. Pamoja na mambo mengine, Waziri Ulega alielezea uhitaji wa kuendelea kuboresha mnyororo wa thamani wa uvuvi hususan zao la dagaa ambalo linavuliwa kwa wingi Nchini Tanzania na kuhusisha jamii kubwa ya wavuvi hususan wanawake na  uhitaji Mkubwa wa kuwekeza katika uzalishaji wa chakula cha samaki kwa ajili ya Ukuzaji Viumbe Maji.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb.), (wa tano kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Sekta ya Uvuvi wa Shirika la Kimataifa la Kilimo na Chakula (FAO). Kulia kwa Mhe.Waziri ni Mkurugenzi wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Manuel Barange,  Msimamizi Mkuu wa Mipango na Sera za Uvuvi, Nicole Franz,  Msimamizi Mkuu wa Mradi wa EAF,  Merete Tandstad,   Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Fish4ACP, Nansen na Steven Ciocca.  Kushoto kwa Mhe. Waziri ni Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo,  Mratibu wa Mradi wa SSF Guidelines, Lilian Inengwe, Afisa wa Ubalozi, Eva Kaluwa na Katibu wa Waziri, Azizi Mhukula.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni