Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo Aprili 2, 2023 amepata fursa ya kutembelea machinjio ya kisasa ya Nguru Hills iliyopo Morogoro katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.
Akiwa katika Mchinjio hiyo Prof. Shemdoe ametembelea sehemu mbalimbali za machinjio hiyo ikiwepo sehemu ya kupumzikia Mifugo kwa masaa ishirini na nne, kabla ya mifugo hiyo kuchinjwa.
"Lengo langu kuja hapa ni kuona ufanisi wa machinjio hii, na nimeridhika na Ubora wa hii machinjio,inavifaa vyote vya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma ya uchinjaji wa Mifugo, tunawaalika wawekezaji wengine wa namna hii ili waje kuwekeza hapa nchini tuwe na mchinjio za kutosha ili tuweza kupeleka nyama yenye viwango nje ya nchi."Alisema Prof.Shemdoe.
Aidha, meneja uzalishaji wa machinjio hiyo Bw. Isaya Mgoo, amemweleza Katibu Mkuu kuwa, Machinjio hiyo inachinja ng'ombe Mia moja (100) kwa siku, Mbuzi na Kondoo (1,000) elfu Moja kwa siku.
Aidha, Machinjio hiyo inaendeshwa kwa umoja kati ya Serikali ya Tanzania kupitia PSSSF, kampuni ya ECLIPSE Investment kutoka Oman Pamoja na kampuni ya BUSARA investment ya hapahapa Tanzania. Pia Katibu Mkuu
ameiagiza NARCO kuiga mfano mzuri wa uwekezaji wa Nguru hills unaoweza kuongeza tija.
Katika hatua nyingine Prof. Shemdoe ameiagiza Bodi ya Nyama nchini kufanya utafiti ili kujua Tasnia ya nyama inachangia kiasi gani kwenye Pato la taifa.
Awali Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Shemdoe amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuimarisha Diplomasia ya Uchumi inayo fungulia wawekezaji milango ya kuja kuwekeza nchini ambapo vijana na akina mama wananufaika na ajira na uchumi unaimarika.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akionyeshwa nyama na Meneja wa Uzalishaji Bw.Isaya Mgoo, ambayo iko katika chumba baridi tayari kwa ajili ya kuipaki kwenye Vifungashio na kuisafirisha kwenda nje ya nchi .Kulia kwa Katibu Mkuu ni Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Bw.John Chasama. Lengo la kutembelea Machinjio hiyo ni kuangali ufanisi na utendaji kazi wake.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa tatu kutoka kulia) akimsikiliza kwa Makini Meneja uzalisha wa Machinjio ya Nguru Hills Bw. Isaya Mgoo (wa kwanza kutoka kushoto) akielezea ufanisi wa Machinjio hiyo.Wengine katika Picha ni Alex Mkenda,Afisa Mifugo kutoka Bodi ya Nyama,John Chasama,Kaimu Msajili bodi ya Nyama Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa Pili kutoka kulia) akionyeshwa eneo ambalo nyama inaning'inizwa tayari kwa ajili ya kupelekwa katika chumba baridi (Cold room).Wengine katika Picha ni Bw.Isaya Mgoo (wa kwanza kulia) John Chasama,Msajili bodi ya Nyama Tanzania na Bw.Alex Mkenda,Afisa Mifugo bodi ya Nyama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni