Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ntime Mwalyambi akifungua akifungua mafunzo ya usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kanda ya Ziwa Tanganyika ambapo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha kuwa kuna kuwa na uvuvi endelevu katika ziwa hilo. Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Sunset mkoani Kigoma. (12.04.2023)
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Festo
Mtanga akiwasalimia washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa rasilimali za uvuvi
Kanda ya Ziwa Tanganyika ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Ziwa
Tanganyika, ambapo amewaeleza kuwa Wizara inaendelea na jitihada za kudhibiti
uvuvi haramu na kutoa elimu juu ya matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi.
Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Sunset mkoani Kigoma.
(12.04.2023)
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ntime Mwalyambi (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kanda ya Ziwa Tanganyika mara baada ya kufungua mafunzo hayo. Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Sunset mkoani Kigoma. (12.04.2023)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni