Nav bar

Ijumaa, 14 Aprili 2023

DKT. MADALLAATEMBELEA VIZIMBA VILIVYOPO KWENYE BWAWA LA DABALO WILAYANI CHAMWINO, MKOANI DODOMA

 

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji viumbe kwenye maji Dkt. Nazael Madalla(wa kwanza kushoto) akionyesha vizimba (havipo pichani) na kutoa maelekezo kwa wahudumu  wa vizimba hivyo vilivyopo kwenye bwawa la Dabalo, kata ya Dabalo, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma 11.04.2023. Alipotembelea na kuona shughuli za ufugaji samaki kwenye bwawa hilo na kutoa elimu ya naman bora ya ufugaji samaki kwenye vizimba.


Mhudumu wa ufugaji samaki kwenye vizimba, kwenye bwawa la Dabalo lililopo Wilaya ya Chamwino, Bw. Hilbert Mwankenje Akilisha chakula samaki walipo kwenye vizimba 21 kwenye bwawa hilo, ambapo Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji viumbe kwenye maji   Dkt. Nazael Madalla(hayupo pichani) alipotembelea 11.04.2023. Kwenye bwawa hilo kuona shughuli zinazoendelea.


Muonekano wa vizimba vilivyopo kwenye bwawa la Dabalo lililopo kata ya Dabalo, Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma ambapo shughuli za ufugaji samaki kwenye vizimba zikiendelea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni