Wafugaji wilayani Tarime wametakiwa kumiliki maeneo na kupanda majani kwa ajili ya malisho ya mifugo yao.
Hayo yamesemwa leo (08.01.2023) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Mashamba Ndaki alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Karekatonga
wilaya ya Tarime mkoa wa Mara baada ya kusikiliza kero zao.
Waziri Ndaki amesema kuwa wafugaji wanatakiwa kubadilika na
kuanza kufuga kisasa na kibiashara kwa kuhakikisha mifugo wanayofuga inapata
malisho ya kutosha kulingana na maeneo wanayoyamiliki pamoja na huduma za
mifugo.
Malisho ni moja ya changamoto kubwa inayowakabili wafugaji
wengi na hivyo kusababisha mifugo kufa hasa kipindi cha ukame. Hivyo wafugaji
wameshauriwa kumiliki mifugo inayoendana na eneo la malisho wanayomiliki.
Vilevile Waziri Ndaki amekemea vikali suala la upigwaji
risasi mifugo linalodaiwa kufanywa na askari wa wanyamapori. Wananchi katika
vijiji vinavyoizunguka Mbuga ya Serengeti wamelalamikia tatizo hilo na hivyo kumuomba
Mhe. Waziri kuwasaidia wafugaji hao.
Aidha, Waziri Ndaki amekemea vikali suala la mifugo kupigwa
risasi kwa kuwa lipo kinyume na sheria zinazolinda mifugo hapa nchini. Hii ni
kutokana na wananchi hao kulalamika kuhusu mifugo yao kupigwa risasi na askari
wa wanyamapori.
Naye Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mhe. Mwita Waitara
amesema kuwa serikali katika jimbo hilo imefanya mambo mengi ya maendeleo
lakini wananchi wameomba suala la alama za mipaka kati ya vijiji na eneo la hifadhi
ya Serengeti liwekwe wazi ili kuondoa migogoro iliyopo sasa kati ya wafugaji na
askari wa wanyamapori.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Kegonga wilayani Tarime mkoani Mara, ambapo amewaeleza
wananchi hao kumiliki maeneo kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kupanda
malisho. (08.01.2023)
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. Kanali Michael Mtenjele akiwasalimu wananchi wa Kijiji cha Karekatongo wilayani humo wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi wilayani humo. (08.01.2023)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni