Nav bar

Jumatano, 25 Januari 2023

SHIRIKA LA HIFADHI YA MAZINGIRA LAWASILISHA MIPANDO YAO KWA WATAALAM WA SEKTA YA UVUVI

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashinba Ndaki (katikati) na Katibu Mkuu wa sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah(kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni kutoka Shirika la Hifadhi Mazingira Duniani "The Nature Conservancy" (TNC) Bi. Lucy Magembe, mara baada ya kumaliza kikao (20.01.2023) cha kumuelezea Mipango ya shirika hilo kwa mwaka 2023 na maeneo watakayofanyia kazi. Kwenye ofisi za Wizara zilizopo Jengo la NBC, Dodoma.


Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah (wa kwanza kulia) akifurahi jambo alipokuwa akimsikiliza muwasilishaji mipango ya  shirika la Hifadhi Mazingira Mkurugenzi wa shirika hilo wa kigoma Bw. Limbu Peter (kushoto) na wataalamu wa sekta ya Uvuvi wakimsikiliza, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Wizara zikizopo Jengo la NBC, Dodoma 20.01.203.


Mkurugenzi wa programu ya Ziwa Tanganyika Kigoma Bw. Limbu Peter (wa tatu kushoto,juu) akiwasilisha kwenye kikao Mipango ya mwaka 2023 ya shirika hilo ambapo shirika litaimarisha usimamizi shirikishi za uvuvi, Ununuzi wa boti za Doria, kuhifadhi maeneo tengefu na amewasilisha kazi ambazo wameshafanya    kwenye ukanda huo. Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za wizara zilizopo Jengo la NBC, Dodoma, 20.01.2023.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekta ya Uvuvi. Dkt. Rashid Tamatamah (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na team kutoka Shirika la Hifadhi mazingira Duniani la The Nature Conservancy (TNC) na wataalamu wa sekta ya uvuvi wa Wizara mara baada ya kumaliza kikao cha kuwasilisha mpango ya Shirila hilo, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Jengo la NBC, Dodoma 20.01.2023.


Mkurugenzi Mkaazi  wa Shirika la Hifadhi mazingira Duniani la The Nature Conservancy Bi. Lucy Magembe (kulia) akimuelezea  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  mhe. Mashimba Ndaki(mb) (katikati) na Katibu Mkuu wa sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah(kushoto) kuhusu Mipango ya Shirika hilo katika sekta ya uvuvi kwa mwaka 2023 ambapo maeneo muhimu ambayo watayafanyia kazi, Ametoa mipango hiyo alipoenda kumtembelea waziri na team ya wataalamu wa shirika hilo  kwenye ofisi za wizara zilizopo Jengo la NBC. Dodoma.  20.01.2023.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na team kutoka shirika la Hifadhi mazingira Duniani "The Nature Conservancy" (TNC) na  (kulia kwake) ni katibu Mkuu wa sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah na wataalamu wa sekta ya uvuvi mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizopo Jengo la NBC, Dodoma, 20.01.2023.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni