Nav bar

Jumatano, 25 Januari 2023

SEKTA YA UVUVI YAWASILISHA TAARIFA YA MAENDELEO YA UJENZI WA BANDARI YA UVUVI

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akifafanua mambo kadhaa baada ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwasilisha kwa wajumbe wa kamati hiyo jijini Dodoma, maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi pamoja na taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23, ambapo Mhe. Dkt. Ishengoma ameielekeza wizara kuhakikisha inasimamia mikakati mathubuti iliyojiwekea ili kufikia malengo. (19.01.2023)


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akiwafahamisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma, mara baada ya kamati hiyo kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi pamoja na taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23, ambapo Mhe. Ndaki amesema wizara itaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha eneo la bandari ya uvuvi linavutia uwekezaji wa viwanda vya kusindika samaki pamoja na kudhibiti uvuvi haramu nchini. (19.01.2023)


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), akiwafahamisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma, hali ya sekta ya uvuvi nchini na namna wizara inavyohakikisha zana zinazotumika katika uvuvi zikiwemo nyavu na taa zinakuwa katika viwango vinavyokubalika, mara baada ya kamati hiyo kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi pamoja na taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23. (19.01.2023)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah, akiwafahamisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma, maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi mara baada ya kamati kupokea taarifa juu ya maendeleo ya ujenzi huo pamoja na taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23. Dkt. Tamatamah amesema ujenzi wa bandari hiyo unatarajia kukamilika Mwezi Septemba Mwaka 2024. (19.01.2023)


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei akiwafahamisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma namna taasisi hiyo inavyofanya tafiti za zana mbalimbali zinazotumika katika uvuvi pamoja na kuainisha madhara ya baadhi ya nyavu ambazo zimekuwa zikiathiri uvuvi wa samaki ambazo zimekatazwa kisheria. Dkt. Kimirei amebainisha hayo baada ya kamati kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi pamoja na taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23. (19.01.2023)


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Stephen Lukanga akiwasilisha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23, ambapo amesema kwa sasa kuna viwanda 32 katika ukanda wa Ziwa Victoria, Pwani na Ziwa Tanganyika ambavyo vinasindika minofu ya samaki, mabondo, mazao ya bahari, dagaa na migebuka. Aidha kamati hiyo imepokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi. (19.01.2023)


Mkurugenzi Msaidizi (Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Merisia Mparazo akiwasilisha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi itakayogharimu Shilingi Bilioni 266 hadi kukamilika kwake Mwezi Septemba Mwaka 2024, na kuongeza kuwa hadi sasa ujenzi umefikia Asilimia 2.5, ambapo ujenzi huo unatekelezwa na mkandarasi Kampuni ya MS China Harbor Engineering kutoka nchini China. (19.01.2023)


Muonekano wa mchoro wa bandari ya uvuvi inayojengwa kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi itakayogharimu Shilingi Bilioni 266 ambapo ujenzi utakamilika Mwezi Septemba Mwaka 2024, katika eneo hilo kutakuwa na huduma muhimu kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za kuhifadhia samaki. Mchoro huu umewasilishwa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma wakati wakipokea taarifa juu ya ujenzi wa bandari hiyo pamoja na taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23. (19.01.2023)


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma walipata fursa ya kuchangia hoja mbalimbali mara baada ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi pamoja na taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23, ambapo wameitaka wizara kuhakikisha inaweka mazingira ya uwekezaji mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bandari hiyo pamoja na kudhibiti uvuvi haramu nchini. (19.01.2023)


Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo zinazohusika na sekta ya uvuvi, wakiwa kwenye kikao wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwenye eneo la Kilwa Masoko katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi pamoja na taarifa ya hali ya utendaji wa viwanda vya kusindika samaki nchini katika nusu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji jijini Dodoma. (19.01.2023)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni