Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda (katikati) akiongea na washauri elekezi wa ndani kutoka kampuni ya Jackson Group, kampuni ya ALG pamoja na watendaji kutoka Sekta ya mifugo (hawapo pichani) wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo mtumba jijini Dodoma lengo likiwa ni pamoja na kupata taarifa za kufanikisha upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa maghala ili kuwezesha uhifadhi wa bidhaa za biashara mtandao Tanzania, Januari 13, 2023
Mshauri elekezi wa ndani kutoka Kampuni ya Jackson Group, Bw. Calvin Twisa akieleza lengo la kufika kwenye Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa watendaji wa Wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za kufanikisha upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa maghala ili kuwezesha uhifadhi wa bidhaa za biashara mtandao Tanzania, Januari 13, 2023 Mkoani Dodoma.
Mshauri elekezi kutoka kampuni ya ALG, Bw. Crustavo Lacetera akiwasilisha mada kwa watendaji wa sekta ya mifugo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kupata taarifa za kufanikisha upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa maghala ili kuwezesha uhifadhi wa bidhaa za biashara mtandao Tanzania, Januari 13, 2023 Mkoani Dodoma.
Daktari Mkuu wa mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Oscar Mbyuzi akichangia hoja wakati wa kikao kifupi cha kupata taarifa za kufanikisha upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa maghala ili kuwezesha uhifadhi wa bidhaa za biashara mtandao Tanzania kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo mtumba Mkoani Dodoma, Januari 13, 2023
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni