Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Wanyama Dkt Asimwe Rwiguza akizungumza kwenye kikao cha kupanga mkakati wa pamoja wa kuendeleza maeneo ya malisho baina ya Wizara na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Watu na wanyamapori (Tanzania People and wildlife-TPW) ambapo lengo la kikao hicho ni kupata taarifa shughuli za uendelezaji wa maeneo ya malisho zinazofanywa na (TPW). Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Wizara Mtumba tarehe. 02.12.2022.
Katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Wanyama Dkt Asimwe Rwiguza (katikati), Mkurugenzi wa uhifadhi Shirika la (TPW) Neovitus Sianga (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt.Angelo Mwilawa (kushoto) wakiwa katika kikao cha kupanga mkakati wa pamoja wa kuendeleza maeneo ya malisho baina ya Wizara na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Watu na wanyamapori (Tanzania People and wildlife-TPW) ambapo lengo la kikao hicho ni kupata taarifa za shughuli za uendelezaji wa maeneo ya malisho zinazofanywa na (TPW). Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba tarehe. 02.12.2022.
Pichani ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maeneo ya Malisho Bwn.Gabliel Bura akizungumzia Malengo ya Wizara katika ujenzi wa miundombinu ya maji ili kuhakikisha mifugo inapata maji yakutosha kwenye kikao kilichokutanisha Wataalam wa Wizara na wakandarasi wanaotekeleza kazi za ujenzi wa miundombinu ya maji ya mifugo ya mabwawa na visima . Kikao hicho kimefanyika ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo Mtumba Jijini Dodoma. (01.12.2022)
Baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa miradi ya maji kwa ajili ya mifugo na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (sekta ya mifugo) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Wanyama Dkt. Asimwe Rwiguza (hayupo pichani). Katika kikao cha Wizara na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji kwaajili ya Mifugo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara Mtumba jijini Dodoma. (02.11.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni