Nav bar

Jumatano, 2 Novemba 2022

 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) katika kikao cha dharura kilichofanyika kwenye ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ambapo lengo kuu la kikao hicho ni utekelezaji wa Sheria ya Usajili, Utambuzi na Ufuatiliaji wa Mifugo kwa njia ya hereni za kieletroniki. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Bw. Tixon Nzunda. (25.10.2022)


Baadhi ya wadau na viongozi wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT)wakiwa katika kikao cha dharula cha utekelezaji wa sheria ya usajili,utambuzi na ufuatiliaji  wa Mifugo hasa swala la uwekaji hereni za utambuzi kwa mifugo. Ombi lao kubwa ni kuiomba wizara iongeze muda wa kukamilisha zoezi hilo pia elimu iendelee kutolewa kwa wafugaji na watoa huduma wawafikie kwenye maeneo yao. Kikao hicho kimefanyika  kwenye ofisi ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki(Mb) iliyopo Mtumba jijini Dodoma leo tarehe ( 25.10.2022).


Mkurugenzi wa huduma za Mifugo wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga (aliesimama) akizungumza na viongozi na wadau wa chama cha mifugo Tanzania (hawapo pichani) katika kikao cha dharula cha utekelezaji wa Sheria ya Usajili, utambuzi na ufuatiliaji wa Mifugo hasa swala la uwekaji hereni za kielekroniki Mifugo. Prof. Nonga  amesema "tarehe 27.10.2022  tutakutana na wabunge, wadau na viongozi wengine wa mifugo kujadiliana swala la utambuzi wa mifugo na changamoto nyingine za mifugo" na kuwasihi wadau wajitokeze kwa wingi. Kikao hicho kimefanyika kwenye ofisi ya waziri wa wizara hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma tarehe 25.10.2022

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni