Nav bar

Jumatano, 2 Novemba 2022

RIPOTI YA TATHMINI YA UTENDAJI WA KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA (NARCO) NA MASHAMBA YA SERIKALI YANAYOZALISHA MIFUGO YAKABIDHIWA

 


Mwenyekiti wa timu ya kutathmini utendaji wa kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Mashamba ya Serikali yanayozalisha Mifugo Prof.Samuel Wangwe (kulia) akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ripoti ya tathmini hiyo katika tukio lililofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo eneo la Mtumba jijini Dodoma leo (24.10.2022). Anayeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia sekta ya Mifugo Bw. Tixon Nzunda.


Mwenyekiti wa timu ya kutathmini utendaji wa kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Mashamba ya Serikali yanayozalisha Mifugo Prof.Samuel Wangwe (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu sekta ya Mifugo Bw. Tixon Nzunda ripoti ya tathmini hiyo katika tukio lililofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo eneo la Mtumba jijini Dodoma leo (24.10.2022).


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akitoa maelekezo kwa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na  Mashamba ya Serikali yanayozalisha Mifugo baada ya kuipitia ripoti ya tathmini ya utendaji wa  kampuni na mashamba hayo leo  (24.10.2022) makao makuu ya Wizara hiyo yaliyopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa timu ya kutathmini utendaji wa kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Mashamba ya Serikali yanayozalisha Mifugo Prof.Samuel Wangwe akiwasilisha ripoti ya tathmini hiyo kwa viongozi na baadhi ya Watendaji wa sekta ya Mifugo ( hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuikabidhi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (hayupo pichani) tukio lililofanyika leo tarehe (24.10.2022) katika ukumbi wa wizara  hiyo uliopo eneo la  Mtumba jijini Dodoma.


Baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ( sekta ya Mifugo) wakisikiliza maelekezo ya  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (hayupo pichani) muda mfupi kabla ya tukio la makabidhiano ya ripoti ya tathmini ya utendaji wa kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na mashamba ya Serikali yanayozalisha mifugo lililofanyika leo tarehe (24.10.2022) Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni