Mjumbe mmoja kwenye kikao cha kutoa maelezo na uhakiki wa fomu za mikopo Mwalimu Dachi kushoto mwenye (kanzu nyeupe) akiomba ufafanuzi baada ya Mkurugenzi Antony Dadu (kushoto)kutoa maelekezo ya ufafanuzi kwa wajumbe kuwa ni mkundi gani yaliyoinishwa kupata mikopo hiyo na kujibiwa kuwa ni manne tu ambayo ni Ushirika wa Wavuvi uliosajiliwa, vikundi vya wavuvi vilivyosajiliwa na Halmashauri,Wavuvi Binafsi wa kubwa,na Makampuni ambapo haya mawili ya mwisho yanajitegemea udhamini leo .(14.10.1022)
Mkurugenzi Masidizi wa Ugani wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Bw.Antony Dadu akitoa maelezo kwenye kikao cha Wadau wa Uvuvi ya ufafanuzi wa masuala muhimu yanayotakiwa katika katika ujazaji wa fomu za maombi ya mikopo ya Boti za Uvuvi,Vizimba vya kufugia Samaki na Boti za kubebea Mwani mita 5 Kamba na taitai ambapo amewambia makundi yanayo pata mikopo hiyo yamegawanyika sehemu nne(4) ambayo ni: Vyama vya Ushirika,Vikundi vya wavuvi vilivyo sajiliwa na Halimashauri ya Pangani,Watu binafsi ambao watajidhamini wenyewe,na Kapuni ambazo wajidhamini na kampuni yao.Aliwagiza wale ambao hawaja kamilisha waendelee na kujaza fomu na waliotayari waziwasilishe kwetu kwa ajili ya kuzihakiki, baadhi ya wavuvi waliuliza matsharti na vigezo baadhi ni pamoja na Barua ya mhutasari wa kikao cha kikundi juu ya kuomba mkopo,Barua ya maombi Cheti cha Akaunti ya banki.Kikao kilifanyika katika kata ya ofisi za Pangani Magharibi Wilaya ya Pangani leo,(14.10.2022).
Afisa Uchumi Bw.Agustine Mshanga kutoka Dawati la Sekta Binafsi, akitoa ufafanuzi kwa wadau wa uvuvi kwenye kikao cha Kuhakiki Fomu za Maombi ya Mikopo ya Boti za Uvuvi (Fibre), zenye ukubwa wa Mita tano (5) kwa ajili ya Kilimo cha Mwani, boti za uvuvi kuanzia Mita Nane (8), Mita kumi (10), Mita kumi na mbili (12) Ambpo amewaeleza Wadau hao masharti ya kuomba mkopo ni pamoja na: Vikundi vya Uvuvi vilivyosajiliwa na Halmashauri,Ushirika wa wavuvi,Wavuvi binafsi ambao watajidhamini kwa mali zao, Makampuni ya Wavuvi watajidhamini, aidha kuwepo na muhtasari wa kikao cha wanachama uliosainiwa, kuwepo na cheti cha usajili wa kikundi toka Halmashuari, andiko la biashara, iwepo leseni ya Uvuvi, ukomo wa madeni na mwisho taarifa ya mikopo.(14.10.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni