Nav bar

Jumatano, 19 Oktoba 2022

SERIKALI KUENDELEA KUPUNGUZA TOZO TASNIA YA KUKU

Na Mbaraka Kambona,


Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara katika sekta ya mifugo na kuhakikisha kwamba mifugo yote ikiwemo kuku inakuwa na Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na Taratibu nzuri zinazosaidia kuboresha biashara hiyo ndani na nje ya nchi.


Nzunda alisema hayo wakati akifungua Maonesho ya Sita ya Kuku na Ndege Wafugwao yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 14, 2022.

 

Wakati akiongea na washiriki wa Maonesho hayo yenye kauli mbiu "Hakuna Zege Bila Kuku!", Nzunda alisema kuwa serikali itaendelea kupunguza na kuondoa baadhi ya tozo ambazo zimekuwa kero na kikwazo katika uzalishaji wa kuku.


"Kwa kushirikiana nanyi wafugaji na wadau wengine wa kuku, washiriki wa maendeleo, Serikali itaendelea kufanyika kazi changamoto zote mlizozibainisha ili tasnia hii iweze kukua na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa wafugaji na nchi kwa ujumla", alisema


Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kutoa elimu ya ufugaji bora wa kuku ikiwa pamoja na kufafanua juu ya Sera , Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayosimamia sekta ya mifugo nchini.


"Ninatoa maelekezo kwa Idara ya Huduma za Mifugo na Bodi ya Nyama kuwa na Programu Maalim kwa ajili ya kutoa elimu ya ufugaji bora na Miongozo yake ili wafugaji waweze kuielewa na kuboresha ufugaji wao", alisisitiza


Katika hatua nyingine alisema kuwa serikali inaangalia uwezekano katika bajeti ya Mwaka ujao wa fedha kutenga bajeti kwa ajili ya kujenga mnada wa  kuku ili kuifanya tasnia hiyo kufanya shughuli zake kisasa na kuondokana na madalali ambao baadhi yao wamekuwa kikwazo kwa wafugaji kupata kipato kinacho stahili.


Maonesho hayo ya kuku na ndege wafugwao yanafanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 14-15, 2022 na yamejumuisha washiriki mbalimbali kutoa katika taasisi za umma, sekta binafsi na makampuni ya kimataifa kutoka ndani na nje ya nchi.

Mtaalamu wa lishe ya  Mifugo kutoka Kampuni ya Koudijs Animal Nutrition Tanzania Ltd, Dkt. Uledi  Kimbavala (kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Tixon Nzunda (kushoto) namna bidhaa za  Kampuni hiyo zinavyowasaidia wafugaji kupunguza gharama na kuongeza uzalishaji alipotembelea Maonesho ya Sita ya Kuku na Ndege Wafugwao yanayofanyika Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 14 -15, 2022.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda (wa pili kulia) akiongea na Maafisa wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) alipotembelea Maonesho ya Kuku na Ndege Wafugwao yanayofanyika, Ubungo Plaza,  jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 14 -15, 2022.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda akiangalia baadhi ya bidhaa za wadau wa tasnia ya kuku alipotembelea Maonesho ya Kuku na Ndege Wafugwao yanayofanyika Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 14 -15, 2022.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda (wa pili kushoto) akiongea na wataalamu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania -TVLA (hawapo pichani) alipotembelea banda la TVLA siku ya tehere 14/10/2022 kwenye Maonesho ya Sita ya Kuku na Ndege Wafugwao yanayofanyika Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 14 -15, 2022.

Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Wanyama kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt Scholastica Doto (kushoto) akitoa maelezo kuhusiana na uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo aina ya kuku pamoja na huduma zinazotolewa na Wakala kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda (wa pili kulia) siku ya tarehe 14/10/2022 

Wataalam kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania –TVLA (Waliopo ndani ya Banda) Dkt. Geofrey Omarch Meneja wa Maabara Kuu ya Mifugo na Dkt Scholastica Doto Mkuu wa kitengo cha Sayansi ya Wanyama wakitoa maelezo kwa wadau wa mifugo kuhusiana na uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo aina ya kuku pamoja na huduma zinazotolewa na Wakala siku ya tarehe 14/10/2022 walipotembelea banda la TVLA kwenye Maonesho ya Sita ya Kuku na Ndege Wafugwao yanayofanyika Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 14 -15, 2022.


Mkuu wa kitengo cha Sayansi ya Wanyama kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt Scholastica Doto (kulia) akitoa maelezo kwa wadau wa mifugo kuhusiana na uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo aina ya kuku pamoja na huduma zinazotolewa na Wakala siku ya tarehe 14/10/2022 walipotembelea banda la TVLA kwenye Maonesho ya Sita ya Kuku na Ndege Wafugwao yanayofanyika Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 14 -15, 2022.


Maonesho ya Sita ya Kuku na Ndege Wafugwao yanayofanyika Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 14 -15, 2022.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni