Nav bar

Jumatano, 19 Oktoba 2022


 Kaimu Mkurugenzi  Halmashauri ya Wilaya ya Magu Bw. Henry James  akifungua kikao chenye lengo la kufanya tathmini na kuona kama wanachama, vikundi, makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na shughuli za uvuvi wamekidhi vigezo vya maombi ya mkopo wa vizimba na maboti yanayotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Ili kuwasaidia kuweza kuvua kwa tija na kuinua kipato cha mvuvi moja mmoja na jamii kwa ujumla kwenye Wilaya hiyo Mkoani Mwanza, Oktoba 13, 2022.

Mkurugenzi msaidizi Idara ya Ukuzaji Viumbe maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Imani Kapinga akiongea na vikundi, wanachama, makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na shughuli ya Uvuvi wakati wa ziara yao wilayani Magu Mkoani Mwanza ya kufanya tathmini ya kuona kama wamekidhi vigezo vya maombi ya mkopo wa vizimba vinavyotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) wilayani hapo Oktoba 13, 2022

Sehemu ya wadau wanaojihusisha na shughuli za uvuvi  waliojitokeza katika zoezi la kufanya tathmini ya taarifa zao kwa ajili  kupata mikopo ya boti na vizimba inayotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kwenye Halmashauri ya Wilaya ya  Magu Mkoani Mwanza, Oktoba 13, 2022

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Emanuel Shekolowa (kushoto) akieleza vigezo vya chama, vikundi, mtu binafsi na makampuni ambavyo wanatakiwa kuwa navyo Ili kuweza kupata mkopo wa boti za kisasa kwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bw. Rashid Mchata (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi yake Mkoani humo Oktoba 13,2022.

Katibu Tawala Wilaya ya Nkasi, Bw. Cosmas Kuyela (katikati) akiongea na watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), mwakilishi kutoka benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB), na wawakilishi kutoka Alpha choice Tanganyika wakati wa kikao kifupi kilichofanyika ofisini kwake chenye lengo la kufanya tathmini ya maombi ya mkopo wa maboti unaotarajiwa kutolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Ili kuweza kuwasaidia wavuvi kuboresha shughuli zao za uvuvi na maisha yao kwa ujumla. Oktoba 13, 2022 Mkoani Rukwa

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa , Bw. Rashidi Mchata (kulia) akiipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kwa hatua nzuri ya kutaka kuwakopesha boti wavuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) ambazo zitaenda kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku za uvuvi na kuweza kunufaika na Uvuvi huo, Oktoba 13, 2022

Sehemu ya wadau wanaojihusisha na shughuli za uvuvi wakimsikiliza kwa makini Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Emanuel Shekolowa (hayupo pichani) wakati akitoa maelezo juu ya aina na ukubwa wa boti zinazotarajiwa kukopeshwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB), Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Oktoba 13, 2022.

Katibu Tawala Wilaya ya Sumbawanga Bi.Christina Mzena (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na mwakilishi kutoka benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika ofisini kwake chenye lengo la kuwasaidia wavuvi kuweza kupata mikopo nafuu ya maboti isiyo na riba Ili kuweza kuvua kwa tija na kuboresha maisha yao, Oktoba 13,2022 Mkoani Rukwa.


Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Eliakim Mniko  akieleza lengo la ziara yao Mkoani Rukwa kwa Katibu Tawala Mkoa, Bw. Rashid Mchata ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya maombi  ya mkopo wa boti za kisasa za uvuvi kwa vyama ,vikundi,makampuni na watu binafsi wanaojihusisha na Uvuvi  ili kuona kama wamekidhi vigezo na kuweza kukopeshwa boti hizo zitakazopelekea kufanya Uvuvi endelevu wenye tija na kusaidia  kuongeza kipato na kupunguza umaskini, kwenye  Halmashauri ya  Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa , Oktoba 13, 2022.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni