Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda akiongea na mkandarasi wa ujenzi wa mnada wa Lupa uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya na mkandarasi wa uchimbaji wa bwawa la Nalalami na Ololeliani Ngorongoro (hawapo pichani) kabla ya kusaini mikataba yao, ambapo amewaeleza nini Wizara inategemea kupata kutoka kwao ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa kazi kwa kuzingati viwango na muda waliopewa. Uwekaji saini umefanyika ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma Septemba 07, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakandarasi wa kampuni mbili tofauti ambazo ni kampuni ya kujenga mnada wa Lupa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya na mkandarasi wa kuchimba bwawa la Nalalami na Ololeliani Ngorongoro mara baada ya zoezi la kusaini mikataba ya ujenzi wa minada na mabwawa lililofanyika ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, Septemba 07, 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni