Nav bar

Ijumaa, 26 Agosti 2022

UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UVUVI HAPA NCHINI.

 


Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wageni kutoka Kampuni ya Relevant na Kampuni ya Carbon Market Exchange inayojishughulisha na biashara ya hewa ya ukaa walipomtembelea leo ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma Agosti 16, 2022. wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni Relevant, Bw. Mohammed Sinani, Wanne  kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu, Carbon Market Exchange kutoka Marekani, Shenna Fortner. Lengo la kukutana na wadau hao ni kuona namna wadau wa sekta ya uvuvi nchini wanavyoweza kunufaika na uuzaji wa hewa ya ukaa katika maeneo ya uhifadhi na kilimo cha Mwani.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akizungumza na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber wakati balozi huyo alipofika katika ofisi za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma na kuelezea nia ya makampuni mbalimbali kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta ya Mifugo kwa kuingia mikataba ikiwemo ya kuwekeza kwenye ranchi za taifa. Aliyekaa kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda. (16.08.2022)

Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber na Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda (kulia), wakati balozi huyo alipofika katika ofisi za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma kuzungumzia masuala mbalimbali ya uwekezaji wa makampuni ya Misri katika Sekta ya Mifugo hapa nchini. (16.08.2022)

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto), akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber, Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Bw. Emmanuel Bulayi na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazael Madalla juu ya uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi, mara baada ya balozi huyo kufika katika ofisi za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma. (16.08.2022)

Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (wa tatu kutoka kulia), Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Bw. Emmanuel Bulayi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazael Madalla (wa kwanza kushoto), mara baada ya mazungumzo juu ya uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi hapa nchini. (16.08.2022)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni