Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia uendelezaji wa rasilimali za Uvuvi Bi. Merisia Mparazo akiongea na wanawake wanaojishughulisha na shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA) (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya masuala ya kijinsia kwa wanawake hao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa the wallet Mkoani Kigoma Agosti 01, 2022.
Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Lilian Ibengwe akiwasilisha mada kwa wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi pamoja na uchakataji wa mazao yake wakati wa mafunzo ya masuala ya kijinsia kwa wanawake hao Agosti 01, 2022 Mkoani Kigoma.
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Upendo Hamidu akiwasilisha mada juu ya jinsi na jinsia kwa wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi na Mazao yake Tanzania wakati wa mafunzo ya masuala ya kijinsia kwa wanawake hao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa the wallet Mkoani Kigoma Agosti 01, 2022.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya masuala ya kijinsia kwa wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi pamoja na uchakataji wa mazao yake wakichangia mada wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa the wallet Mkoani Kigoma Agosti 01, 2022.
Moja ya kikundi kilichokuwa kikijadili masuala ya kijinsia na usawa kwa wanawake wanaojihusisha na uchakataji wa mazao ya Uvuvi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa the wallet Mkoani Kigoma Agosti 01, 2022
Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Lilian Ibengwe akieleza lengo la kuanzishwa kwa TAWFA ikiwa ni pamoja na kuwaleta wanawake pamoja Ili waweze kujadili changamoto zao na kushiriki katika shughuli mbalimbali kwa pamoja wakati wa mafunzo ya masuala ya kijinsia kwa wanawake wanaojihusisha na shughuli za uchakataji wa mazao ya Uvuvi, Agosti 02, 2022 Mkoani Kigoma.
Afisa Mfawidhi ubora na masoko Kanda ya bahari ya Hindi, Bi. Jovice Mkuchu akiwasilisha mada kwa wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya masuala ya kijinsia kwa wanawake hao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa "the wallet" Mkoani Kigoma Agosti 02, 2022.
Mtaalam wa masuala ya jinsia kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la umoja wa Mataifa (FAO) Nchini Ghana, Bi. Clara Park akiwasilisha mada ya usawa wa kijinsia kwa wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa "the wallet" Mkoani Kigoma Agosti 02, 2022.
Sehemu ya wanawake wanaojihusisha na shughuli za uchakataji wa mazao ya Uvuvi wakiwasilisha majibu ya mazoezi waliyopewa Ili kupima uelewa wakati wa mafunzo ya masuala ya kijinsia (picha ya juu kulia) ni Mchakataji wa Mazao ya Uvuvi Mkoa wa Kigoma Bi. Mwamisa Khalid ( picha ya chini kulia) ni Katibu wa Coastal Women Fishworker Organization (COWOFO) Bi. Pili Kuliwa, Agosti 02, 2022 Mkoani Kigoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni