Nav bar

Jumapili, 14 Agosti 2022

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA MAONESHO YA NENANANE AGOSTI 3, 2022

 


Afisa Mifugo Bi. Hellen Mtambo (kushoto) na Afisa Utafiti Bi. Grace Masolwa (katikati) kutoka Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani wakimpa maelekezo mdau wa ufugaji juu ya namna ya kuingia kwenye mfuko wa kielektroniki wa "M-Kilimo" mara baada ya mdau huyo kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yanapofanyika maonesho ya NaneNane kanda ya kati leo. (03.08.2022)


Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Sikudhani Mponda (kulia) akitoa maelekezo kwa mdau wa Uvuvi kuhusu hatua za ufugaji wa samaki mara baada ya mdau huyo kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yanapofanyika maonesho ya NaneNane kanda ya kati leo (03.08.2022).


Mkufunzi kutoka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA). kutoka kampasi ya Kibirizi Kigoma, Bw.Meshack Maguru (wa pili kulia) akitoa elimu ya ufugaji bora wa samaki kwa njia ya mabwawa kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (3.8.2022)


Mmiliki wa Kampuni ya Farm43 Africa,  inayozalisha na kusambaza mbegu za nguruwe aina ya TN70, Bw.Aron Mwasile ambaye pia ni mdau wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi akionesha chakula bora cha nguruwe kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (3.8.2022)


Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani (Uvuvi) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Antony Dadu (wa pili kushoto) akitoa elimu ya ufugaji bora wa samaki kwa njia ya mabwawa kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya (3.8.2022)


Meneja wa  shamba la serikali la uzalishaji wa ng”ombe wa maziwa Kitulo, Bw. Gerald Mashurano akitoa maelezo ya kitaalam kuhusu ufugaji bora wa ng”ombe wa maziwa kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (3.8.2022)


Afisa Mifugo  mkuu kutoka idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani (DRTE) Bi. Atupele Mohamed akitoa maelezo kuhusu huduma za ugani kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya wakulima nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini  Mbeya. (3.8.2022)


Mkurugenzi msaidizi idara ya Huduma za Mifugo, Sehemu ya Udhibiti wa Magonjwa yaenezwayo na wadudu, Dkt. Benezeth Lutege akiwaonesha wadau hereni za kielektroniki kwa ajili ya utambuzi wa mifugo kwenye maonesho ya wakulima nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. (3.8.2022)


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bi Fatma Mwassa akisaini kitabu cha wageni leo (03.08.2022) muda mfupi baada ya kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane kinda ya Mashariki yanayoendelea Mkoani Morogoro.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi Fatma Mwassa (wa tatu kulia) akiangalia viatu vilivyotengenezwa kwa zao la Ngozi kutoka kampuni ya GAMO Enterprises, alipoenda kutembelea leo tarehe 03.08.2022 kwenye banda la wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki  yanayoendelea kufanyika Morogoro.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Fatma Mwassa, akikagua mabanda ya  Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea kufanyika Morogoro leo tarehe 03.08.2022.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni