Nav bar

Jumatatu, 18 Julai 2022

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA MAONESHO YA 46 YA KIBIASHARA (SABASABA) - JIJINI DAR ES SALAAM

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb) ametembelea Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl J.K Nyerere jijini Dar es Salaam na hapa ni kwenye jengo la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambapo Mhe. Ulega amepata wasaa wa kutembelea banda hilo na kuona shughuli zinazofanywa na Tume hiyo. (05.07.2022)


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akisaini kitabu cha wageni cha Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es Salaam *#TANZANIA: SEHEMU SAHIHI PA BIASHARA NA UWEKEZAJI (05.07.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah akisainik kitabu cha wageni kwenye Banda la Zanzibar (KARIBU ZANZIBAR) alipofanya ziara ya kutembelea mabanda kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah akisalimiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima walipokutana kwenye Banda la Wizara ya Kilimo wakiwa kwenye ziara ya kutembelea mabanda kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. (06.07.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah akipata ufafanuzi kutoka kwa Mtafiti Msaidizi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Bw. Samson Goodluck (kushoto) kuhusu mashine inayotumika kupima maziwa bila kutumia kemikali (LAB IN THE BOX) wakati Dkt. Tatamah alipofanya ziara ya kutembelea mabanda kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. (06.07.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah akisalimiana na Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) Bw. Shaka Hamdu Shaka walipokutana wakiwa kwenye ziara ya kutembelea mabanda kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. (06.07.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah akipatiwa maelezo kutoka kwa maafisa wa Bodi ya Maziwa Tanzania juu ya usimamizi wa Sekta ya Maziwa nchini unaofanywa na bodi hiyo alipofanya ziara ya kutembelea mabanda kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.(06.07.2022)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah akiongea na waandishi wa habari kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mabanda kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. (06.07.2022)


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) akisaini kitabu cha wageni cha Bodi ya Maziwa Tanzania alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) katika Viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar Es Salaam. (06.07.2022)


Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya akipokea maelezo kutoka kwa watumishi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kuhusiana na taasisi hiyo inavyofanya kazi alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mifugo na Uvuvi Julai kwenye kilele cha Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) katika viwanja vya Mwl. J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam. (07.07.2022)

Afisa Mifugo, Bi. Senorina Mwingira kutoka Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) akitoa elimu kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Bright Angels waliotembelea banda la Bodi ya Nyama kwenye maonesho ya Kimataifa ya 46 ya biashara katika viwanja vya Mwl. Nyerere yanayoendelea jijini Dar Es Salaam. (09.07.2022)


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Five Star Agrovet Bw. Francis Pentzel akitoa elimu juu ya utafiti uliofanyika kwenye zao la mwani na kuweza kupata mbolea asilia kwa kutumia zao hilo kwa wananchi waliofika kwenye banda la Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar Es Salaam. (09.07.2022)


Picha ikionesha wananchi wakipata elimu ya namna ya kutengeneza chakula cha mifugo kwa kutumia njia za kisasa kwa gharama nafuu walipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.k Nyerere (Sabasaba) jijini Dar Es Salaam. (08.07.2022)


Wananchi waliofika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa ufugaji samaki namna ya kufuga samaki kwa kutumia bwawa la kisasa la kuhamishika lenye uwezo wa kuhifadhi samaki 350 hadi 400. (08.07.2022)


Meneja Masoko wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Bw. Emmanuel Mnzava akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi juu ya upatikanaji wa mbegu bora za ng'ombe zinazozalishwa na kampuni hiyo wakati wa Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es Salaam. (08.07.2022)


Afisa Ufundi kutoka kampuni ya Nasha Bw. Musa Ngametwa akitoa elimu juu ya fursa zilizopo kwenye ukuzaji viumbe maji kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es Salaam. (06.07.2022)


Wananchi mbalimbali wamefika katika banda la Kampuni ya Triram na kupata elimu juu ya uzalishaji na uuzaji wa mbegu za samaki nchini walipotembelea Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere jijini Dar es Salaam. (06.07.2022)


Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Bi. Esther Mulyila (kulia) akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu samaki aina ya jodari pezi njano, kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) katika viwanja vya Mwl. J.k Nyerere jijini Dar es Salaam. (05.07.2022)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni