Nav bar

Jumamosi, 4 Juni 2022

WAVUVI MKOANI TANGA WAPATIWA MAFUNZO YA UCHAKATAJI SAMAKI KWA NJIA VIDEO.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikishirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) inaendelea kutoa mafunzo kwa njia ya video kuhusu uchakataji Samaki kwa wavuvi wa mkoa wa Tanga.


Akifungua mafunzo hayo leo 31.05.2022. Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Afisa Uvuvi wa mkoa huo Bw. Issa Hatibu ameishukuru Wizara na Shirika la (FAO) kwa jitahada za kuiendeleza sekta ya uvuvi kwa kutoa mafunzo kwa wavuvi waliopo Tanga ili kuweza kupata samaki wenye ubora na kipato cha Halmshauri kiweze kuongezeka pamoja na kipato cha mkoa na hatimaye kitaifa.


BW. Hatibu amewataka wavuvi kuyafuata mafunzo hayo ili kuweza kuyafanyia kazi na kuweza kuongeza mnyororo wa dhamani ya uvuvi mkoani Tanga,


Naye, Mshauri wa Shirika la Chakula na kilimo Duniani, Dr. Patrick Kimani amesema elimu inayotolewa kwa njia ya video kwa kuonyesha Shughuli za uvuvi mdogo ambapo mojawapo ni njia ya kukausha samaki pamoja na samaki kwa kutumia chanja.


Pia Dr. Kimani ameongezea kwa kusema ili kuongeza dhamani ya samaki mbinu nyingine ya kuvua dagaa ni kuvua kwa njia ya madumu, ambapo mbinu hii inatumika baharini na wavuvi ili kuwezesha kuweka ubora wa samaki bila ya kuleta hasara yoyote, uharibifu au kupoteza dhamani.


kwa upande wake, Afisa Uvuvi Mwandamizi, Bi Upendo Hamidu amesema mafunzo haya ni muendelezo wa utekelezaji wa muongozo wa hiyari wa kusimamia uvuvi nchini ambapo unaangazia maswala mbalimbali lakini hasa katika mnyororo wa dhamani wa mazao ya uvuvi ambako ndiko kuna kuwa na changamoto.


Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa utekelezaji wa Mwongozo wa kimataifa wa kuendeleza uvuvi mdogo, Bw. Yahya akichangia mada kuhusu faida ya kuwa na vikundi kwenye kuongeza mnyororo wa  dhamani ya mazao ya uvuvi. wakati wa mafunzo kwa njia ya video ya uchakataji wa samaki, yaliyofanyika katika ukumbi wa maktaba ya Mkoa wa Tanga, 31 Mei 2022.

Mshauri wa Shirika la chakula na kilimo Duniani(FAO) Dr. Patrick Kimani akitoa elimu kwa wadau juu ya  namna bora ya uchakataji samaki na kuwwza kupata samaki wenye ubora katika masoko ya nje wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba ya mkoa wa Tanga, 31 Mei 2022.


Mratibu wa Mradi wa Small Scale Fisheries (SSF) Bi. Lilian Ibengwe akielekeza jambo kwa wadau (hawapo pichani) wakati wa mafunzo kwa njia ya video ya uchakataji samaki, ambayo yamefanyika katika ukumbi wa maktaba ya mkoa wa Tanga, leo 31.05.2022.

Sehemu ya wadau wa sekta ya uvuvi, walioshiriki mafunzo ya  uchakataji samaki wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na muwezeshaji (hayupo pichani) yaliyofanyika katik ukumbi wa maktaba ya mkoa wa Tanga, 31 Mei 2022.

Washiriki wa mafunzo kwa njia ya video kuhusu uchakataji Samaki wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo hayo mkoani Tanga, wakiwa nje ya ukumbi wa maktaba ya Mkoa wa Tanga, leo 31 mei 2022.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni