Nav bar

Ijumaa, 3 Juni 2022

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA UWASILISHAJI WA BAJETI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) akiwasilisha hotuba ya mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2022/23. (25.05.2022)


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akiwasilisha bungeni jijini Dodoma, taarifa ya kamati kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na maoni ya kamati kuhusu makadirio ya mapato na matumzi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23. (25.05.2022)


Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakigonga meza kuashiria kukubaliana na hoja mbalimbali ambazo Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), (hayupo pichani) wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma, hotuba ya mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2022/23. (25.05.2022)


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), wakati akiwasilisha hotuba ya mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2022/23, ambapo wizara imeliomba bunge kuidhinisha Shilingi Bilioni 268,252,007,000. (25.05.2022)

MATUKIO KATIKA PICHA

Picha za Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) na Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega (Mb), wakiwa katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma na kupiga picha na wageni waliofika kumsikiliza Waziri Ndaki akiwasilisha ndani ya bunge hilo hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23. (25.05.2022)






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni