Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza mafunzo ya kuhamasisha zoezi la utambuzi, usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo katika mikoa yote ya Tanzania, moja ya mikoa hiyo ambayo mafunzo hayo yanatolewa ni mkoa wa Ruvuma.
Akiongea katika Ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya songea, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Pololet Mgema ametoa pongezi kwa Wizara kwa kuona umuhimu wa kutoa Elimu kabla ya zoezi hilo kufanyika, mafunzo hayo yamefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma tarehe 10.12.2021.
Mgema amesema Mfumo wa utambuzi na Ufuatiliaji Mifugo Tanzania unasimamiwa kwa Sheria ya Usajili, utambuzi na Ufuatiliaji Mifugo Na. 12 ya mwaka 2020 na kanuni zake za mwaka 2011, na kwa Mkoa wa Ruvuma, Halmashauri ziko kwenye hatua tofauti ya maandalizi ya kutekeleza zoezi hilo.
"Nitoe rai kwa wafugaji wote walioko katika Mkoa wa Ruvuma kutoa Ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi la utambuzi kwa njia ya hereni kwa Mifugo yenu", amesema Mgema.
Aliongezea kwa kusema ni muhimu wafugaji Waelewe zoezi hilo na kuchangia utekelezaji wake, na hakuna uchaguzi kama tunataka kuelendelea kuwa wafugaji wa zama hizi za sasa na zijazo.
Aidha, aliomba Wizara kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo, Viongozi wa Halmashauri, chama cha wafugaji na wataalam wa Mifugo ili kutatua changamoto ya migogoro baina ya wakulima na wafugaji, kwani wafugaji wengi hawana maeneo ya kuchungia.
Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya jamii ya Mifugo, Dkt. Stanford Ndibalema alisema mwaka 2017, wizara ilianza na kutambua Mifugo kwa kutumia alama za chapa ya moto, ambazo kila kila Kijiji kilikua na namba, lakini zoezi hilo liligubikwa na changamoto ya alama kufutika na malalamiko ya kuharibu Ngozi, na ya kukiuka ustawi wa wanyama kwakuwa ule moto unaumiza wanyama.
Ndibalema aliongeza kwa kusema kwa kuona hivyo serikali ikaja na utaratibu mzuri wa kutumia mfumo kielektronik unaofuatwa kwa kuvalisha Mifugo hereni kwenye sikio.
Naye Afisa Mifugo kutoka Halmashauri ya Mbinga, Haruna Masige ametoa wito kwa wafugaji wawe kupokea zoezi hilo la utambuzi kwakuwa lina faida kubwa ikiwapo kuzuia wizi na inatoka Fursa kwa serikali kupanga Mipango thabiti kwa nchi nzima,
Pia, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Mbinga, Grace Quitine alikiri kupokea mafunzo hayo na anaimani mafunzo hayo ya tawezesha viongozi kwenda kutoa Elimu kwa wafugaji ili naweza kusajili Mifugo yao na ili kuleta faida ya kuweza kupata Masoko hata nje ya nchi na kuweza kuongeza pato la nchi kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema
akiwa na timu ya watoa mafunzo ya kuhamasisha zoezi la utambuz, usajili na
ufuatiliaji wa Mifugo kutoka Wizarani, walipoenda kumtembelea ofisini kwake, ameongea
namna ya sekta ya Mifugo inavyochangia katika pato la Mkoa wa Ruvuma na kuweza
kuongeza pato la Nchi, (kushoto) ni Mkuu wa kitengo cha TEHEMA, Baltazar
Kibola, Mhasibu Martin Machibya tarehe
10.12.2021.
Mgeni Rasmi,
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, ambae pia ni Mkuu Wilaya ya Songea, Pololet
Mgema, akitoa hotuba katika Ufunguzi wa mafunzo na kuhamasisha zoezi la
Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo kwa Mikoa ya Tanzania bara katika
Mkoa wa Ruvuma, kwa washiriki waliohudhuria mafunzo mafunzo hayo (hawapo
pichani), kwenye ukumbi wa Songea Club, ltarehe
10.12.2021.(kulia) Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Jamii
ya Mifugo, Dkt. Stanford Ndibalema, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni