Nav bar

Jumatatu, 10 Januari 2022

WADAU WA TASNIA YA MAZIWA WASHAURIWA KUWA NA VIPAUMBELE VICHACHE VYA UTEKELEZAJI.

SERIKALI imesisitiza haja ya kuja na vipaumbele ambavyo vitachagiza sekta ya mifugo hususani tasinia ya maziwa kuchangia Pato la Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Aidha, imeelezwa kuwa asilimia 86 ya maziwa wanayozalishwa hapa nchini hayako katika soko rasmi jambo ambalo linachangia walaji kutokuwa na imani na bidhaa hiyo hivyo kuchangia uagizaji wa maziwa kutoka nje ya nchi

Haya yameelezwa leo Jijini hapa na Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dk George Msalya wakati wa kufungua kikao kazi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (sekta ya Mifugo) kilichojumuisha wadau mbalimbali wa Tasnia ya Maziwa wanaokutana kwa lengo la kubainisha vipaumbele ambavyo vitawekezwa ili kuleta matokeo chanya na kuleta mafanikio yanayoonekana.

Hatua ya kujadili vipaumbele vya uwekezaji ni katika kutekeleza mradi wa kujenga uwezo kwa ajili ya utekelezaji na ufuatiliaji wa Mpango Kabambe wa Sekta ya Mifugo.

Alisema sekta ya mifugo imeendelea kukua na kuifanya Tanzania kushika nafasi ya pili barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi ambapo kwa sasa kuna ng'ombe milioni 33.9.

Alisema kwa sasa mchango wa Pato la Taifa kwa Mifugo ni asilimia 7 na kuwa sekta hiyo inauwezo mkubwa wa kuongeza mchango zaidi huku zaidi ya kaya milioni 2 zinajihusisha na shughuli za ufugaji.

“Tunahitaji uwekezaji wenye tija, lakini tunataka idadi kubwa ya mifugo tuliyonayo ichangie zaidi katika uchumi wa nchi katika Pato la Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja au kaya moja moja."

Alisema katika kikao cha Oktoba kilibainisha maeneo 10 ya uwekezaji na kusisitiza kuwa ili kuwa na mafanikio ya haraka ni vyema kuwa na vipaumbele vichache kama vitatu Ili kupata mchango wa haraka.

Aidha, Dk Msalya alisema kwa upande wa tasinia ya maziwa inaendelea kukua na inakuwa kwa asilimia 2 hali ambayo bado ni ndogo, huku ikichangia Pato la Taifa kwa asilimia 2, na inachangia sekta ya mifugo kwa asilimia 30

“Bado tuko chini pamoja na kuwa na idadi kubwa ya mifugo hivyo kunahitaji uwekezaji mkubwa."

Aidha, Dk Msalya alisema tasinia ya maziwa inakabiliwa na changamoyo ya kuwa na asilimia 86 ya maziwa wanayozalishwa na kuwa katika soko lisilo rasmi wakati uchakataji wa maziwa ni asilimia tatu ya maziwa yanachakatwa kati ya lita bilioni 3.3 zinazozalishwa hivyo kuhitaji nguvu na uwekezaji katika eneo hilo.

“Maziwa yasiyo katika mfumo rasmi ubora wake unakuwa haujulikani hivyo kufanya walaji kutokuwa na imani na bidhaa hiyo, hivyo nitoe wito watu kufuata takwa la sheria kwa kuingiza maziwa mengi kwenye soko rasmi."

“Kwa sasa kuna vituo 220 vya kukusanya maziwa lakini bado maziwa hayakusanywi maziwa na hayafiki kwenye vituo, najua kuna changamoto kadhaa, sasa kikao hiki kiangalie namna ya kuja na suluhisho ili maziwa mengi yaingie kwenye mfumo rasmi tuwe na maziwa bora ambayo yanawafikia walaji na wayatumie bila kuwa na mashaka yoyote."

Dk Msalya alisema pia kuna haja ya kuweka nguvu katika uwekezaji ili kuimarisha viwanda vya ndani.

Dkt.Msalya alisema pia kuna haja ya kuweka nguvu katika uwekezaji ili kuimarisha viwandda vya Maziwa nchini ambavyo viko 104 na vinahitaji malighafi ya kutosha.



Picha ya pamoja ya washiriki wa kikao kazi cha siku moja cha kujadili Mrejesho wa fursa ya vipaumbele vilivyoibuliwa katika kikao kazi kilichopita kwa lengo la kupata vipaumbele mbele vichahe kati ya vingi na kuelekeza nguvu ya kutosha katika hivyo vichahe kwa mafanikio chanya tarajiwa, katika viwanja vya Royal Village Hoteli Jijini Dodoma.   (14 .12 .2021). 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni