Mtendaji Mkuu wa
Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akisoma
taarifa ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kuhusu miradi ya utafiti
inayotekelezwa na Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) Kibaha kwa ufadhili wa Tume
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) wakati wa ziara fupi
iliyofanywa na Waziri wa elimu, Sayansi na teknolojia ,Mhe. Prof. Joyce
Ndalichako ili kuona utekelezaji wa miradi hiyo katika Taasisi hiyo iliyopo
Kibaha, mkoani Pwani julai 3, 2021.*
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (katikati)
akiongea na viongozi pamoja na watumishi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari
Tanzania (TVLA) wakati wa ziara fupi iliyofanyika kwenye ofisi za
Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani. Julai
3, 2021*
Mtendaji Mkuu wa
Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi (kulia)
akimtembeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako
(Mb) kwenye majengo ya Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya
Kibaha Mkoani Pwani. Julai 3, 2021*
Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akipata maelezo ya
namna kazi za uthibiti ubora wa chanjo zinavyofanyika kwa kutumia vifaa na
mashine vilivyopatikana kwa ufadhili wa COSTECH kwenye maabara ya Taasisi
ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani. Julai 3,
2021*
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni