Na Mbaraka Kambona,
Taasisi
za fedha nchini zimeipongeza Serikali kwa maamuzi ya kulifufua Shirika la Uvuvi
Tanzania (TAFICO) na kulipa tena nafasi ya kuweza kusimamia mnyororo wa thamani
wa zao la Samaki huku wakiahidi kutoa mtaji ili kuliimarisha shirika hilo.
hayo
yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Japhet
Justine alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kumaliza
kikao kazi cha kujadili maeneo ya uwekezaji ya Shirika la Uvuvi Tanzania
(TAFICO) kilichofanyika jijini Dodoma Februari 2, 2021.
Akiongea
kwa niaba ya Viongozi wengine wa taasisi za fedha waliohudhuria kikao hicho,
Justine alisema kuwa TAFICO ni shirika kubwa linaloshikilia mnyororo mzima wa
thamani wa samaki hivyo kufufuliwa kwa shirika hilo kutawasaidia wavuvi kuwa na
masoko ya uhakika.
“Tunaipongeza
Serikali kwa maamuzi haya makubwa ya kulifufua shirika hili, na sisi
tumewahakikishia kushirikiana nao katika kutoa mitaji ambayo itaanzia kwa
TAFICO yenyewe na wale wote wanaojihusisha katika mnyororo huu wa thamani
ikiwemo wavuvi, wasafirishaji na watengeneza barafu,” alisema Justine
Alisema
kwa sasa kuna wananchi zaidi ya laki mbili (200,000) wanaojihusisha na uvuvi na
kuongeza kuwa hao wote wataenda kuwafungamanisha katika mnyororo huo wa
thamani.
Aliongeza
kuwa kufufuliwa kwa shirika hilo kutaongeza fedha za kigeni, uhakika wa kupata
masoko makubwa ya kimataifa ambayo yataleta mikataba ya kibiashara
itakayowarahisishia wadau walioko katika sekta ya uvuvi kukopeshwa mitaji.
“Tunaamini
mabenki ambayo yalikuwa yanapata shida kupata mikataba ya kuweza kuwapatia
wafanyabiashara wadogowadogo mitaji, sasa kwa kupitia mikataba ya TAFICO
italeta ahueni kubwa na kupunguza madhila yaliyokuwa yanazuia mabenki kutoa
mitaji,” alifafanua Justine
“Sisi
kama taasisi za fedha ikiwemo mabenki, Kituo cha Uwekezaji na Mifuko ya
Pensheni tumekubaliana tutaweka nguvu kwa pamoja kuhakikisha miradi yote kumi
(10) iliyobuniwa na TAFICO inayoangazia kutengeneza mazingira thabiti ya uvuvi
inasimama kwa awamu nyingine tena ili tija ya shirika hilo iweze kuonekana,”
alisisitiza Justine
Naye,
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah alisema
kuwa uendeshaji wa shirika hilo kwa awamu hii utakuwa ni wa ubia kati ya
Serikali na sekta binafsi.
Aliongeza
kuwa kwa miaka mingi tangu uhuru haukuwepo uwekezaji katika bahari kuu huku
akisema kuwa ni mategemeo yao kuwa uwekezaji ukianza katika uvuvi wa bahari kuu
samaki wataongezeka mara tatu zaidi ya wanaopatikana sasa.
Dkt.
Tamatamah alisema kuwa shirika hilo likianza kufanya kazi sekta ya uvuvi
itaimarika na pia litasaidia kuzuia uvuvi haramu na kulinda rasilimali za uvuvi
katika bahari kuu.
Taasisi
zilizoshiriki kikao hicho ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Benki ya
CRDB, Benki ya NMB, na Benki ya Posta (TPB).
Nyengine
ni Kituo cha Uwekezaji, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati)
akiongea na Washiriki wa kikao kazi cha kujadili maeneo ya uwekezaji ya Shirika
la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kilichofanyika jijini Dodoma Februari 2, 2021.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uvuvi (WMUV), Magese Bulayi akifafanua jambo katika kikao kazi cha
kujadili maeneo ya uwekezaji ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)
kilichofanyika jijini Dodoma Februari 2, 2021.
Sehemu
ya Washiriki wa Kikao kazi cha kujadili maeneo ya uwekezaji ya Shirika la Uvuvi
Tanzania (TAFICO) wakipitia nyaraka mbalimbali katika kikao hicho
kilichofanyika jijini Dodoma Februari 2, 2021.
Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Japhet Justine akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha kujadili maeneo ya uwekezaji ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kilichofanyika jijini Dodoma Februari 2, 2021.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa sita kutoka
kulia-mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi za
fedha na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha
kujadili maeneo ya uwekezaji ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)
kilichofanyika jijini Dodoma Februari 2, 2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni