Washiriki wa mafunzo ya ukaguzi wa rasilimali
ya vyakula vya mifugo kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo
ya Afisa Mifugo Mtafiti Mkuu kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania
(TVLA), Bi. Wende Maulaga (kushoto) wakati akitoa mafunzo hayo kwenye Maabara
ya TVLA jijini Dar es salaam. (07/01/2021)
Afisa Mtafiti Mifugo
Mwandamizi, kitengo cha Upimaji Ubora na Usalama kutoka Wakala ya Maabara ya
Veterinari Tanzania (TVLA), Dkt. Scholastica Doto akionyesha na kutoa elimu ya
namna mashine ya kupimia madini kwenye vyakula vya mifugo inavyofanya
kazi kwa washiriki (hawapo pichani) wa mafunzo ya ukaguzi wa rasilimali ya
vyakula vya mifugo walipotembea maabara ya TVLA jijini Dar es salaam.
07/01/2021.*
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utambuzi na
Huduma za Uchunguzi kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA),
Dkt. Chanasa Mpelumbe akimvalisha kitambulisho mmoja wa washiriki wa mafunzo ya
ukaguzi wa rasilimali ya vyakula vya mifugo kutoka Tanga Bw. Mustafa
Khalifan baada ya kufunga mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika kwenye ukumbi
wa TVLA jijini Dar es salaam. 07/01/2021.*
*Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Vyakula vya Mifugo,
Idara ya Uendelezaji malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo kutoka Wizara
ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Rogers Shengoto akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi
ambaye ni Mkurugenzi wa Utambuzi na Huduma za Uchunguzi kutoka Wakala ya
Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Chanasa Mpelumbe na washiriki wote
(hawapo pichani) wa mafunzo ya ukaguzi wa Rasilimali ya Vyakula vya Mifugo
wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika kwenye ukumbi wa TVLA
jijini Dar es salaam. 07/01/2021*
Mkurugenzi wa Utambuzi na Huduma za Uchunguzi kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dr. Chanasa Mpelumbe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam waliotoa mafunzo ya ukaguzi wa Rasilimali ya Vyakula vya Mifugo pamoja na washiriki wa mafunzo mara baada ya kuwakabidhi vitambulisho na kufunga mafunzo hayo kwenye ukumbi wa TVLA jijini Dar es salaam. 08/01/2021*
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni