Nav bar

Jumatatu, 21 Desemba 2020

MAFUNZO YA UCHUNAJI NGOZI KWA WASHIRIKI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ILALA.

 


Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe,  Idara ya Uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Gabriel Bura akitoa maelezo mafupi ya umuhimu wa mafunzo ya uchunaji ngozi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo hayo ya siku moja kwa wachunaji ngozi wapatao 74 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yaliyofanyika Mvuvi House jijini Dar es salaam, 21/12/2020.



Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uchunaji ngozi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Msaidizi wa  Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Idara ya Uzalishaji na Masoko, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Gabriel Bura (hayupo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika Mvuvi House jijini Dar es salaam, 21/12/2020.





Mgeni rasmi, Afisa Biashara Mkuu, kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Thabiti Massa akisisitiza washiriki kuzingatia mafunzo yote waliofundishwa ili kupata ngozi bora kwa matumizi ya viwanda ndani na nje ya nchi kabla ya kuwapatia leseni wachunaji ngozi wapatao 74 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yaliyofanyika Mvuvi House jijini Dar es salaam, 21/12/2020. Kulia kwa mgeni rasmi ni mshauri wa masuala ya Mifugo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Odetha Muchunguzi.



Mgeni rasmi, Afisa Biashara Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Thabiti Massa akimkabidhi leseni mmoja wa washiriki wa mafunzo ya uchunaji ngozi Bw. Juma John baada ya kufunga mafunzo hayo ya siku moja kwa washiriki wapatao 74 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yaliyofanyika Mvuvi House jijini Dar es salaam, 21/12/2020



Mgeni rasmi, Afisa Biashara Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Thabiti Massa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na washiriki wa mafunzo ya uchunaji ngozi wapatao 74 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yaliyofanyika Mvuvi House jijini Dar es salaam, 21/12/2020.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni