Meneja wa benki ya NMB
kanda ya Ziwa Mashariki Bw. Sospeter Magese (katikati) akitoa maelezo kwa
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kuhusu kiasi cha Mkopo
kilichotolewa na benki hiyo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi mpaka sasa ikiwa
ni sehemu ya ziara ya Mhe. Mpina aliyoifanya kwenye mabanda mbalimbali yaliyopo
kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (06.08.2020).
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (kushoto) akipata maelezo kuhusu sheria na kanuni
mbalimbali zinazoongoza sekta za mifugo Uvuvi kutoka kwa Mwanasheria wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi Bi. Irene Lukindo (kulia) mara tu baada ya kufika kwenye
mabanda ya Wizara hiyo ikiwa ni sehemu yake aliyoifanya kwenye mabanda
mbalimbali yaliyopo kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (06.08.2020).
Kutoka kulia
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
watu Zakariyya Kera ndc na Mkurugenzi wa Ukuzaji viumbe maji Dkt. Nazael Madala
wakipata maelezo kwenye banda la Umoja wa wakulima wa mbogamboga na matunda
(TAHA) wakati wa Ziara ya Mhe. Mpina kwenye mabanda mbalimbali yaliyopo kwenye
viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (06.08.2020).
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimpa maelezo
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (wa tatu kutoka kulia) huku
wakielekea yalipo mabanda ya sekta ya Uvuvi wakati wa Ziara ya Mhe. Mpina
kwenye mabanda mbalimbali yaliyopo kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (06.08.2020).
Afisa Uvuvi Mwandamizi
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Pudensia Panga akitoa maelezo kwa wadau
waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane
yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (06/08/2020)
Mkufunzi kutoka Wakala
ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Bw. Ijumaa Bakari akitoa maelezo ya namna
wanavyofanya kazi kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na
Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi
Mkoani Arusha. (06/08/2020)
Mchumi Mkuu kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Sophia Mlote akitoa maelezo kwa wadau
waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane
yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (06/08/2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni