Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es
Salaam Mhe. Godwin Gondwe (Kushoto) wakikagua bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa
kwa kutumia (ukili/ukindu) mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya
Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki
yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane Mkoani Morogoro. (05.08.2020)
Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akishuhudia chanjo sita za mifugo zinazozalishwa
hapa nchini chini ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA)
inayosimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakati alipotembelea Maonesho ya
Nanenane Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani
na Morogoro, yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane Mkoani Morogoro. Pembeni
yake ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam Mhe. Godwin Gondwe.
(05.08.2020)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah
Ulega (Wa pili kutoka kulia) akiwa na mwenyeji wake katika Maonesho ya Nanenane
Kanda ya Mashariki Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam Mhe. Godwin
Gondwe (Wa kwanza kutoka kulia) wakati wakikagua bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa hapa nchini zinatokana na mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi baada
ya Naibu Waziri Ulega kufika katika Viwanja vya Nanenane Mkoani Morogoro
kujionea maonesho hayo. (05.08.2020)
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam Mhe. Godwin Gondwe akifurahia kumshika samaki aina ya kambakochi baada ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kumtaarifu namna samaki huyo alivyo na thamani kubwa katika masoko ya kimataifa wakati walipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Morogoro, yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane Mkoani Morogoro. (05.08.2020)
LINDI
Mkuu wa Wilaya ya
Masasi, Mhe. Selemani Mzee (aliyevaa suti nyeusi) akisaini kitabu cha wageni
wakati alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya
Nanenane Kanda ya Kusini katika viwanja vya Ngongo - Manispaa ya Lindi. Kulia
ni Mtafiti Mkuu wa Mifugo kutoka TALIRI Naliendele, Abel Mtambuki.
(05.08.2020)
Mkuu wa Wilaya ya Masasi,
Mhe. Selemeni Mzee akiangalia viatu vya ngozi kwa mmoja wa wajasiriamali kutoka
Lungwana Shoe Products, Amedeus Thadeus (aliyevaa tisheti nyekundu) wakati
alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane
Kanda ya Kusini katika viwanja vya Ngongo - Manispaa ya Lindi.
(05.08.2020)
Afisa Uvuvi
Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji Kanda ya Kusini Lindi, Hassan Mchwapi akitoa
maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Selemani Mzee wakati alipotembelea
mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya
Kusini katika viwanja vya Ngongo - Manispaa ya Lindi. (05.08.2020)
DODOMA
Mgeni rasmi, Kaimu
Mkuu wa Mkoa, Dodoma, Mhe. Mwanahamisi Munkunda(kulia) akijadiliana jambo kuhusu
bidhaa ya dagaa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof.
Elisante Ole Gabriel alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika
Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Mkoani Dodoma
Agosti 5, 2020.
Mgeni rasmi, Kaimu
Mkuu wa Mkoa, Dodoma, Mhe. Mwanahamisi Munkunda (katikati) akiongea na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kilimo, Mifugo na Ufugaji Tanzania (TALAS), Felix Filangali (kulia)
alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane
yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma Agosti 5, 2020. Kushoto ni
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Profesa Elisante Ole
Gabriel.
Mgeni rasmi, Kaimu
Mkuu wa Mkoa, Dodoma, Mhe. Mwanahamisi Munkunda (wa pili kushoto) akiwa
ameshika kiatu, moja ya bidhaa inayotengenezwa na Kampuni ya Simons,
alipotembelea banda la Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane
yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma Agosti 5, 2020. Wa
kwanza kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof.
Elisante Ole Gabriel.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba fupi kabla ya
kumkaribisha Mgeni rasmi kuongea na Wananchi katika Maonesho ya Nane Nane
yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma Agosti 5,
2020.
ARUSHA
Mkuu wa Wilaya ya Longido na Mgeni Rasmi wa siku ya leo Bw. Frank James Mwaisumbe akipanda farasi mara baada ya mashindano ya mifugo kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (05/08/2020)
Daktari wa Mifugo
kutoka kituo cha Uhimilishaji NAIC, Bw. Elibariki Njiku akitoa maelezo kwa
wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya
nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha
(05/08/2020)
Afisa Uvuvi kanda ya Kaskazini, Bi. Gloria Patiri
akitoa maelezo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha
(05/04/2020)
SIMIYU
Afisa kutoka Kitengo
cha Mazingira, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Magreth Domick akitoa maelekezo
kwa wateja waliofika kwenye banda lao kwa ajili ya kupata huduma (05.08.2020)
kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Afisa kutoka Kitengo
cha Mazingira, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Omary Mafitah (kushoto) akitoa
maelekezo kwa wateja waliofika kwenye banda lao kwa ajili ya kupata huduma (05.08.2020) kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Kaimu Mkurugenzi wa
Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TARILI)kanda ya nyanda za juu kisini
-Uyole,Mbeya, Dr. Edwin Chang'a akiongea na waandishi wa habari kuhamasisha
wadau na wananchi wote kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye
maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale Mkoani
Mbeya ( 05/08/2020)
Afisa Mifugo kutoka shamba la Mifugo Sao Hill mafinga Mkoa wa Iringa Domitila Barnos akitoa maelezo kuhusu malisho bora kwa mdau aliyetembelea mabanda ya wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maadhimisho ya maonyesho ya nanenane yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya tarehe 05.08.2020.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni