Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Isabela Chilumba akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kwenye mabanda ya wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maadhimisho ya maonyesho ya nanenane yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya John Mwakangale tarehe 04.08.2020.
Afisa uvuvi kutoka kituo cha maendeleo ya
ufugaji samaki Ruhila Mkoa wa Ruvuma Justine Ndayeze akitoa maelekezo jinsi ya
kutengeneza chakula cha samaki kwa mdau alipotembelea katika maadhimisho ya
Kilimo,Mifugo na Uvuvi(nanenane) Nyanda za juu kusini Mbeya tarehe
04.08.2020.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Isabela Chilumba
(aliyevaa suti nyeusi) akipata picha ya pamoja na vijana kutoka HEIFER
International ambao wanajihusisha na mambo ya teknolojia ya ufugaji na ufugaji bora,
alipotembelea katika mabanda ya wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maadhimisho ya
maonyesho ya nanenane yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya John
Mwakangale mkoani Mbeya tarehe 04.08.2020.
Afisa Uvuvi,
Bw. George Mbena akielezea na kuonesha teknolojia rahisi ya ufugaji samaki kwa
wadau waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya
nanenane kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu (5/8/2020).
Wafugaji kutoka Halmashauri za wilaya za
Butiama na Maswa wakihamasisha wafugaji wenzao kupitia vyombo vya habari
kutumia teknolojia ya uhimilishaji ng’ombe baada ya wao kufanikiwa kuongeza
idadi ya mifugo kutokana na uhimilishaji. Wafugaji hao wametoa wito kwa
wafugaji wenzao kutembelea maonesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja
mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu ili
kupata huduma hiyo bure.
Mkufunzi wa Wakala ya
Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA-Nyegezi), Revocatus Charamila (mwenye kofia
nyeupe) akitoa maelezo kuhusu mafunzo yanayotolewa na taaisisi hiyo ikiwa ni
pamoja kuwaonesha teknolojia rahisi za ufugaji wa samaki kwa wadau
waliotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane
kitaifa yanayoendelea mkoani Simiyu (5/8/2020).
Msambazaji wa madini
ya Mifugo kutoka kampuni ya usambazaji wa madini (JOSERA), Bw. Elirehema Laizer
akitoa elimu ya madini na umuhimu wa madini kwa mifugo kwa mdau aliyetembelea
banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea
kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (04/08/2020)
Kaimu Msajili wa Bodi
ya Nyama Tanzania, Bw. Imani Sichalwe akipata maelezo kutoka kwa daktari wa
mifugo NAIC, Bw. Elibariki Njiku alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya
nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha themi Mkoani Arusha (04/08/2020)
Mtaalam wa Sungura kutoka kampuni ya SAORE, Bi.
Zaina Ramson akitoa elimu ya ufugaji wa sungura kibiashara kwa wadau
waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane
yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi jijini Arusha (04/08/2020)
DODOMA
Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Huduma za
Ugani(WMUV), Dkt. Angello Mwilawa(kushoto) akimuonesha mbegu bora za malisho
Mkurugenzi Mtendaji, Kampuni ya Kilimo, Mifugo na Ufugaji wa Samaki
Tanzania(TALAS), Yvonne Robben walipokutana katika banda la Wizara ya Mifugo na
Uvuvi kwenye Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya
Nzuguni, Mkoani Dodoma Agosti 4, 2020.
Afisa Mauzo, Kampuni
ya Pimak, Ally Pande akitoa maelezo kwa Wadau wa mifugo kuhusu huduma
zinazotolewa na kampuni hiyo katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye
Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Mkoani Dodoma
Agosti 4, 2020. Wa kwanza kulia ni Afisa kutoka Bodi ya Nyama, Irene
Nselela.
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo
Tanzania(TALIRI), Neema Urassa(kulia) akitoa maelezo kuhusu ufugaji wa Sungura
kwa Wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho
ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma Agosti 4,
2020
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni