Hayo yamesemwa na Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina wakati akizindua Baraza la Veterinari (VCT),
Bodi ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo (LITA) na Bodi ya Hifadhi za Bahari na
Maeneo Tengefu (MPRU) jijini Dodoma.
Waziri Mpina amesema kuwa
kumekuwepo na tabia ya kukamata ng’ombe bila kuwapatia huduma muhimu ikiwemo
maji na malisho hali inayosababisha mifugo mingi kufa huku mingine ikiuzwa
kiholela na kusababisha hasara kwa wafugaji.
Pia alisema kuwa haiwezekani mifugo
inakufa kwa siku moja halafu mfugaji anapewa cheti cha kifo wakati Wizara
haijui mifugo imekufa na nini.
“Mifugo 942 imekufa kwa siku
moja halafu mfugaji anapewa cheti cha kifo, Wizara haijui mifugo imekufaje,
jambo hili ni hujma na Baraza la Veterinari mhakikishe mnalishughulikia hili na
wahusika wachukuliwe hatua”, alisema Waziri Mpina
Katika hatua nyingine, Waziri
Mpina amelitaka baraza hilo kuchukua hatua kali watu wa wasiokuwa watalaam wa
magonjwa ya mifugo “vishoka” ambao wanajihusisha na utoaji tiba.
“Ni marufuku kwa vishoka
kutoa huduma ya afya ya wanyama, na tukikutana nae, sio kosa tu la kulipa faini,
bali itabidi twende kwenye fidia ambapo atalipa fidia kwa hasara aliyosababisha
kwa mfugaji”, alisisitiza Waziri Mpina.
Aidha, Waziri Mpina amelitaka
baraza hilo kuhakikisha katika mapendekezo ya maboresho ya sheria ya baraza
wahakikishe suala la udhibiti wa vishoka linawekwa. Pia ameagiza wanachi
waendelee kupewa elimu ili waweze kuwatambua vishoka. Vilevile Waziri Mpina
ameliagiza baraza kuwafutia usajili na kuwazuia madaktaria wa mifugo ambao hawajahuisha
taarifa zao kwenye daftari la usajili na kuhakikisha hawajihusishi na utoaji wa
huduma.
Awali Waziri Mpina alitoa rai
kwa bodi ya Uhifadhi wa Rasilimali za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) kutangaza
shughuli wanazofanya Pamoja na vivutio vilivyopo katika bahari na maziwa ili
kuvutia shughuli za kitalii na kuongeza mapato.
Pia ameiagiza Bodi hiyo
kuhakikisha inaweka mkakati na kuweka alama za mipaka yakiwemo maboya katika
maeneo tengefu ili kuepuka migogoro na wananchi.
"Bodi ikaweke mipaka
inayotambulika kama maboya katika Maeneo Tengefu na sio kukamata ovyo wavuvi na
kusema wako ndani ya eneo la hifadhi wakati mipaka hakuna, hii itasaidia
kupunguza migogoro”, alisisitiza Waziri Mpina.
Kwa upande wa Bodi ya LITA,
Waziri Mpina ameitaka bodi hiyo kwenda kushughulikia changamoto zilizopo
ikiwemo ya upungufu na ubovu wa miudombinu kama maabara, mabweni, maktaba na
nyumba za walimu. Pia bodi hii imetakiwa kuhakikisha kuwa kuanzia Septemba –
Octoba wafugaji 1500 wanapatiwa elimu ya ufugaji bora kwa kuingizwa darasani
katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizindua Bodi ya Hifadhi za
Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Bodi ya Wakala ya Vyuo vya Mafunzo Tanzania
(LITA), na Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) katika ukumbi wa kambarage
jijini Dodoma. (06.07.2020)
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwapongeza wateuliwa
wapya na wale waliomaliza mda wao wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), Bodi
ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) na Bodi ya Wakala ya Vyuo vya
Mafunzo ya Mifugo (LITA) katika ukumbi wa kambarage jijini Dodoma. (06.07.2020)
wakati wa uzinduzi wa bodi hizo.
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti Mstaafu wa LITA
Dkt. Jeremiah Haki mara baada ya kusoma taarifa hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi
ya Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Bodi ya Hifadhi za Bahari
na Maeneo Tengefu (MPRU) na Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) iliyofanyika
jijini Dodoma (06.07.2020)
Baadhi ya wajumbe
wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga
Mpina (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi ya Wakala ya Vyuo vya Mafunzo
ya Mifugo (LITA), Bodi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) na Baraza
la Veterinari Tanzania (VCT) Jijini Dodoma (06.07.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni