Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akisaini kitabu cha wageni wakati
alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwenye Maonesho ya
44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere,
Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo (5/7/2020)
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akipokea Zawadi kutoka kwa
Florence Mahimbo wa Kampuni ya Bigfish wakati alipotembelea Maonesho ya 44 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, Barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo (5/7/2020)
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akipata maelezo kutoka kwa
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI), Bi. Neema Urassa
wakati alipotembelea Monesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo
(5/7/2020)
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akitoa ushauri kuhusu ufugaji wa
Samaki kwa kutumia matanki wakati alipotembelea banda la SUMA JKT kwenye
Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl.
Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo (5/7/2020)
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiwa na Afisa Masoko wa
Kampuni ya AKM Glitters, Jackson Kaheza alipotembelea Kampuni hiyo inayofanya
shughuli zake jijini Dar es Salaam mapema leo Julai 5, 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel akisaini Kitabu cha Wageni
alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Kimataifa
ya 44 ya biashara (Sabasaba) yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mwl. Nyerere,
Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai 5, 2020. Kushoto anayeshuhudia
ni Mratibu wa Maonesho wa Wizara hiyo, Mary Yongolo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akimsikiliza Mtangazaji wa
TBC1, Vumilia Mwasha wakati wa Mahojiano katika banda la Wizara ya Mifugo na
Uvuvi lililopo katika Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya biashara ya (Sabasaba)
yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mwl. Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Da es
Salaam leo Julai 5, 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiangalia
malisho ya mifugo katika banda la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) lilipo
ndani ya banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Kimataifa ya 44
ya biashara (Sabasaba) yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mwl. Nyerere, Barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai 5, 2020. Kulia ni Mtafiti kutoka TALIRI,
Neema Urassa na wa pili kulia (aliyevaa kofia ya njano) ni Mkurugenzi wa TALIRI
Kanda ya Mashariki, Dkt. Zabron Nziku.
Makatibu Wakuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi wakisalimiana punde walipokutana leo Julai 5, 2020 katika
Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya biashara (Sabasaba) yanayofanyika katika Uwanja
wa Mwl. Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel na Kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatama.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya AKM Glitters inayofanya shughuli zake
jijini Dar es Salaam. Prof. Gabriel alitembelea Kampuni hiyo mapema leo Julai
5, 2020 kwa lengo la kuona shughuli wanazofanya. Kampuni hiyo inajishughulisha
na ufugaji wa kuku aina ya Kuroiler, Kutotolesha Vifaranga na Kusaga vyakula
vya kuku.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni