Mgeni rasmi, Waziri wa
Biashara na Viwanda, Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali akitoa hotuba katika
hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (sabasaba)
iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam. (13.07.2020)
Waziri wa Biashara na Viwanda
kutoka Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali (katikati waliokaa) akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi waliokuwa meza kuu katika hafla ya kufunga Maonesho ya 44
ya kimataifa ya biashara (sabasaba) iliyofanyika. Wa kwanza kulia waliosimama
ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari, Tanzania, ambaye pia
alikuwa Muwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Furaha Mramba. (13.07.2020)
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Maabara ya Veterinari, Dkt. Furaha Mramba akishiriki kuimba Wimbo wa Taifa muda
mfupi baada ya mgeni rasmi kuwasili katika hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya
Kimataifa ya biashara (sabasaba) kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam. (13.07.2020)
Mkuu wa Utawala JKT, Col.
Julius Kadawi (kushoto) akieleza jambo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo
na Uvuvi katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (sabasaba)
yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam. Kulia anayemsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo
na Huduma za Ugani (WMUV), Bezia Rwongezibwa. (13.07.2020)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI), Dkt. Ismael Kimirei alikuwa ni miongoni mwa
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya Kimataifa
ya biashara (sabasaba) kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa
jijini Dar es Salaam. (13.07.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni