Nav bar

Jumatano, 15 Julai 2020

MAONYESHO YA 44 YA KIMATAIFA YA BIASHARA "SABASABA" 2020


Mdau wa Ufugaji wa Chaza, Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Abdallah Mkwamba (kushoto) akitoa maelezo kuhusu samaki aina ya Nguva (aliyewekwa hapo chini) kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (12.07.2020)



Fundi Sanifu Mwandamizi, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Kassian Haule (kushoto) akiwaonesha wananchi vidani vilivyotengenezwa kwa madini ya Lulu walipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (12.07.2020)



Afisa Mifugo, Idara ya Uzalishaji na Masoko (WMUV), Happyness Lyimo (aliyeshika mbegu za malisho ya mifugo) akitoa ufafanuzi kuhusu mbegu hizo kwa wadau wa mifugo waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtaalam wa Mifugo, Idara ya Huduma za Mifugo, Stanslaus Mchonde. (12.07.2020)



Afisa Mifugo Mtafiti Mkuu (WMUV), Felista Kimario (kushoto) akieleza jambo kwa mdau wa mifugo aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (12.07.2020)



Mtaalam wa Samaki, NASHA Aqua Fish Services, Masumbuko Nzingula (kushoto) akimsikiliza mmoja wa wadau wa ufugaji wa samaki aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya biashara (sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (12.07.2020)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni