Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah jana (09.11.2019) amekutana na
wabunge wa majimbo ya Ukanda wa Pwani jijini Dodoma kujadili jinsi ya
kuendeleza na kuimarisha kilimo na biashara ya zao la mwani.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa warsha hiyo Katibu Mkuu Dkt. Tamatamah amesema zao la mwani limekuwa
mkombozi mkubwa kwa wakulima na wafugaji wadogo wadogo wa maeneo ambayo hapo awali
walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi na kilimo.
Aidha amesema baada ya
mafanikio kuonekana kwenye ukuaji wa zao la mwani kampuni nyingi zimeanza
biashara ya kulima na kusafirisha zao hilo nchi za nje.
Pamoja na hayo, imeelezwa
kuwa kutokana na changamoto mbalimbali uzalishaji umeshuka na Tanzania sasa
hivi ni nchi ya tatu, katika uzalishaji ambao umeshuka hadi kufikia tani 918
kwa mwaka 2018/2019 ukilinganisha na wastani wa tani 1,395 kwa mwaka 2017/2018,
tani 1,197 kwa mwaka 2016/2017 na tani 1,500 kwa miaka ya 2000.
Aidha ametoa sababu za
kushuka kwa uzalishaji wa zao la mwani ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi,
ukosefu wa mitaji na wawekezaji makini, ununuzi wa mwani usiofuata utaratibu na
kuleta migogoro baina ya wawekezaji na wazalishaji na kutokuwepo kwa soko la
ndani.
Dkt. Tamatamah amewataka
wabunge hao kutoka Ukanda wa Pwani kutoa maoni yatakayohakikisha biashara ya
zao la mwani inafanyika kikamilifu kwa amani, uaminifu na kufuata sheria
zilizopo ili wadau wote wanaojishughulisha kwenye mnyororo wa thamani wa zao
hilo waweze kunufaika.
”Kwa upande wa serikali
kupitia Wizara yetu tumechukua hatua mbalimbali kufanya tafiti zinazopunguza changamoto
zilizopo na kuwajengea uwezo wakulima ikiwemo fursa za mikopo na kuongeza kasi kuwatafutia
soko na kuona wakulima wa mwani wanaongeza kiwango cha ulimaji na uwezo wa
ubunifu.” Amesema Dkt. Tamatamah.
Aidha amefafanua kuanzishwa
kwa Dawati la Sekta Binafsi kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuwakutanisha wakulima
na wafugaji wadogo wadogo na taasisi za kifedha na imefanya vizuri na sasa
kujikita zaidi kwenye zao la mwani.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi ( Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah akielezea umuhimu na faida za
zao la mwani kwa namna ambayo limekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima na wafugaji
wadogo wadogo wakati akifungua warsha ya wabunge kutoka ukanda wa Pwani kwenye
ukumbi wa NBC jijini Dodoma ili zao hili liweze changia zaidi pato la Taifa.
(09/11/2019
Baadhi ya wabunge na wawakilishi wa wabunge
kutoka katika ukanda wa Pwani wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi ( Uvuvi ) Dkt. Rashid Tamatamah ( hayupo pichani) wakati
akifungua warsha ya kujadili namna ya kuendeleza na kuimarisha kilimo na
biashara ya zao la mwani katika ukumbi wa NBC jijini Dodoma. (9/11/2019)
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni