VIWANDA VINAVYOTUMIA MALIGHAFI ZA MIFUGO KUTAMBULIWA ILI KUFIKIA UCHUMI WA KATI
Serikali imewataka maafisa mifugo wote nchini katika maeneo yao ya kazi kufuatilia idadi ya viwanda vinavyotumia malighafi ya mifugo ambavyo vinafanya kazi pamoja na ambavyo havifanyi kazi kufahamu changamoto zake ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi na viwanda hivyo vianze kufanya kazi kuendana na azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda Mwaka 2025. Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amebainisha hayo jana (27.10.2019) katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara wakati alipotembelea kiwanda cha kuchakata mazao ya mifugo cha Rotiana Social Investment ambacho kwa sasa hakifanyi kazi na baadhi ya mitambo yake kuharibika na vifaa vingine kudaiwa kuibiwa na baadhi ya watu waliokuwa wakikisimamia kiwanda hicho. Prof. Gabriel amesema lengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni kuhakikisha inasimamia vyema azma ya serikali kuhakikisha viwanda vya malighafi za mifugo vinafanya kazi na kutaka maafisa hao wa mifugo kushirikiana na maa...