SERIKALI YATEKETEZA
TANI 8 ZA NYAMA ZILIZOKWISHA MUDA WA MATUMIZI.
Serikali kupitia
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeteketeza tani 8 za nyama kutoka maeneo mbalimbali
mkoani Arusha ambazo zimebainika zimekwisha muda wake wa matumizi na hazifai
kwa matumizi ya binadamu.
Tukio hilo la uteketezaji
wa nyama limefanyika tarehe (22.03.2019) eneo la Njiro likiongozwa na Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) ambapo tani hizo za nyama
zilikamatwa wakati wa Operesheni Nzagamba II Viwandani.
Kufuatia
tukio hilo la uteketezaji wa bidhaa za mifugo na mazao yake, Waziri Mpina alisema
hatuta endelea kuangalia uozo ukiendelea kufanyika na tutahakikisha tunaendelea
kudhibiti uiongizaji holela wa mazao hayo na zilizokwisha muda wake wa
matumizi.
“Operesheni yetu
hii ni ya kila siku na tunaendelea kutokomeza mazao ya mifugo yanayoingia
nchini bila vibali hatutafikia mwisho mpaka jambo hili likamilike, alisema
Waziri Mpina”.
Waziri Mpina
alisema, hakuna mtu atakayewekeza kwenye nchi yetu kama hatuwezi kusimamia
vizuri masoko yetu ya ndani na kuwalinda wenye viwanda vyetu.
“Ukiruhusu taifa
likaenda namna hii ni nani mwekezaji wa nchi yeyote atakayekuja kuwekeza kwenye
nchi ambayo inaruhusu mtu kuingiza bidhaa bila utaratibu, alisemaWaziri Mpina
Waziri Mpina alisema,
rasilimali za nchi lazima wananchi wanufaike nazo, mifugo haiwezi kuchukuliwa
na mtu yeyote ikavushwa na kutumika na watu wengine bila sisi kulipia
ushuru kwa mujibu wa sheria.
“Lazima wananchi,
wawekezaji na wafanyabiashara wote wafuate sheria na taratibu mbalimbali za
nchi yetu zinazozuia kuingiza bidhaa ambazo hazijathibitishwa ubora wake na
kukaguliwa”. alisema Waziri Mpina
Serikali haitachoka
kuendelea kuchukua hatua kali na watendaji wa serikali lazima mhakikishe mnakua
makini maeneo yote ya mipaka yetu, na kuteketeza huku kunaniuma lakini hatuwezi
kuacha kuendeleza uovu uendelee kutokea operesheni na doria hizi hazitafika
mwisho hadi hapo hali itakapokuwa imerejea, alisisitiza Waziri Mpina.
Nikiwa kama Waziri
mwenye dhamana ya Wizara yangu ya mifugo na uvuvi ningependa watu wanaofanya
biashara ya mifugo na mazao yake wanufaike na watajirike, alisisitiza Waziri
Mpina.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo amesema wamegundua Waziri Mpina
amefanya mambo mengi na kuna vitu vizuri ambavyo wizara imefanya kwa maslahi ya
ndani ya nchi.
“Serikali ya Mkoa
wa Arusha tunakuunga mkono na tupo bega kwa bega kushirikiana na wale ambao
hawataki kufuata sheria na maslahi ya nchi na tunashukuru waziri umejiridhisha
na mzigo huo umeonekana na kufukuliwa, watu waache tabia ya kujichukulia sheria
mkononi, alisema Bw. Gambo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni