Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2018

KIKAO KAZI CHA WAZIRI MH. LUHAGA MPINA NA WASINDIKAJI WAKUBWA WA MAZIWA NCHINI.

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Joelson Mpina (Mb) amekutana na Kampuni kubwa za usindikaji wa maziwa nchini (Tanga Fresh, ASAS,MILCOM NA AZAM) leo tarehe 12/11/2018 jijini Dodoma. Lengo la kikao kazi hicho ilikuwa ni kujadili mikakati ya uongezaji wa Usindikaji wa maziwa kwenye Kampuni kubwa za Maziwa nchini.   Nataka Ifikapo tarehe 12/12/2018 mkakati wa ushirikiano uwe umekamilika na kusainiwa kati ya Kampuni za Wasindikaji wa Maziwa na Dawati la Sekta Binafsi, alisema Mh.Waziri Luhaga Mpina. Mhe. Mpina aliwaelekeza Wakuu wa Idara na Vitengo kila mtu kwa upande wake kulitumia na kulisimamia dawati katika kutekeleza Mikakati iliyopangwa.   Mkakati huu unaenda kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa asilimia 84.7 kwa mwaka, alisema Mpina. Tunazindua mkakati wa dawati tarehe 15/12/2018 na kwenda kuwakabidhi mitamba 350 kwa wafugaji wa Chama Kikuu-Tanga kama shukurani kwa jitihada za wenzetu wa TADB, Mpina. Serikali imefanya jitihada kubwa k...

MAKATIBU WAKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA WATUMISHI WA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI.

Picha
Kufuatia kikao cha watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kilichofanyika Leo tar 7/11/2018 katika ukumbi wa VETA DODOMA Katibu Mkuu Mifugo ahamasisha yafuatayo:- Ushirikiano kati ya watumishi ni jambo la Msingi sana ili kuweza Kufanikisha shughuli zetu za kila siku pia ni lazima tufanye kazi kwa kujituma. Changamoto siyo sehemu ya maisha ila changamoto ndiyo maisha yenyewe, kwa hiyo tunazitumia hizo changamoto kama fursa. Wakurugenzi   na   wakuu  wa vitengo  jitahidini sana kuwasikiliza mnaowaongoza ,na   kuwasimamia na kubwa   zaidi kujali maslahi yao. Nataka Wizara hii iende kwa kasi sana ,Idara ya Uzalishaji na Masoko Ikiwa kama Operating Engine kwa sababu ndiyo yenye activities nyingi sana Pia napenda kuwataarifu   rasmi   kuwa Dr. Angelo Mwilawa   kuanzia   sasa nimemteua   kuwa Mkurugenzi Rasmi  wa Idara ya Ugani na mafunzo (DRTE) hapo awali alikuwa anakaimu.  KMU asisitiza Sekta...

PROJECT LAUNCHING WORKSHOP, 07 NOVEMBER,2018. AT MORENA HOTEL DODOMA.

Picha
Prof. O. Gabriel receives inception report from Hon. Minister of Agriculture Dkt. Charles Tizeba Ongoing speech from Permanent Secretary Picture with Minister of Agriculture, Permanent Secretary, AGRA team and ESRF members

NEW ZEALAND KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), amekutana na Balozi wa New Zealand Nchini Tanzania Mike Burrell Ofisini kwake leo tarehe 06/11/2018 jijini Dodoma. Tumekuwa tukishirikiana vyema kati ya Nchi ya Tanzania na New Zealand katika kupata madume bora ya Ng’ombe 6 kule kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) kilichopo UsaRiver jijini Arusha ambayo yamechangia uzalishaji wa mbegu bora kuongezeka zaidi, alisema Mh. Ulega. Mh.Ulega alisema tutasaidiana katika upande wa ufugaji wa samaki, ambapo wenzetu wako mbele zaidi katika masuala ya Ukuzaji viumbe kwenye maji. “ Our President Dkt. John P. Magufuli is trying so hard to ensure that, our environment in Tanzania is getting better and better”. Say’s Ulega. Vilevile Mhe. Ulega alisema kunahitajika watu wa kwenda kusoma katika kada ya Sayansi ambapo kwa sasa bado tunapeleka watu wachache katika fani hiyo. Kwa upande wake balozi Mike alisema, tunahitaji Ushirikiano na Tanzana katika kuwekeza ...

WAKURUGENZI WAPYA WATAMBULISHWA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante Ole. Gabriel leo atambulisha Wakurugenzi wapya katika kikao cha Wakuu wa Vitengo na Idara kilichofanyika katika Ukumbi wa NBC Leo. # Prof. O. Gabriel, alisisitiza Wakurugenzi kujifunza kwa watu na kuwa na Ushirikiano. #KM aliwataka Wakurugenzi kuwa wabunifu katika kazi zao ili kuinua Sekta. # Prof. aliwaomba Wakurugenzi kukabiliana na changamoto zilizopo na kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuzitatua. # Alisisitiza kujenga utamaduni wa Kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa Ushirikiano. Katibu  Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel ampongeza na kumkaribisha Kaimu Mkuu mpya wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini Bi. Rehema ,bulalina, leo katika ukumbi wa NBC KM Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel ampongeza na kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa Idara ya Huduma za Mifugo Dkt. H. Nonga, Leo katika ukumbi wa NBC KM Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel  ampongeza na kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa I...

KATIBU MKUU ATEMBELEA SOKO LA SAMAKI FERRY KUKAGUA UJENZI WA VYOO:

Picha
Leo Katibu Mkuu wa Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama alikwenda kuangalia utekelezaji wa ujenzi wa vyoo 24 hiyo ikiwa ni katika hatua za utekelezaji wa ahadi za Mh. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina alipotembelea sokoni hapo na kubaini mapungu yaliyopo ikiwemo. 1. Uchakavu wa majengo 2. Upungufu wa vyoo; 3. Kujaa kwa mchanga katika bahari: na 4. Uchakavuwa jokofu la kuhifadhia samaki Ambapo alisema kuwa Wizara yake itaingilia kwa kuchukua hatua za haraka katika hayo na kuagiza mara moja kwa ujenzi wa vyoo 24 ambavyo vitapunguza msongamano sokoni hapo. Katibu Mkuu wa Uvuvi, Dkt. Rashidi Tamatamah ametembelea soko la samaki Ferri- Kivukoni kuangalia ujenzi wa vyoo 24 ambavyo vitapunguza msongamano katika soko hilo. Katibu Mkuu Uvuvi, akielekea eneo la ujenzi akiambatana na Meneja wa soko  Bw. Mkuu Anje Katibu Mkuu Uvuvi akiwa katika eneo la Ferry  Katibu Mkuu akiwa na Meneja wa soko hilo akifafanua jambo sokoni hapo Choo ambacho ki...