Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2018

TAHARIFA KWA UMMA KUHUSU TAHADHARI YA MLIPUKO WA UGONJWA WA HOMA WA BONDE LA UFA (RVF)

Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF) ni ugonjwa hatari kwa binadamu na mifugo hususan ng’ombe, mbuzi, kondoo na ngamia ambao husababishwa na virusi jamii ya Bunyaviridae . Wanyama huambukizwa kwa kuumwa na mbu aina ya ‘Aedes”. Binadamu hupata ugonjwa kwa kushika au kula nyama ya mnyama aliyeambukizwa na virusi vya ugonjwa huo Katika   siku za hivi Mamlaka ya Hali ya Hewa Kenya, Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE) na Shirika la Afya   Duniani (WHO) wametoa taarifa za matukio ya ugonjwa wa   Homa ya Bonde la Ufa (RVF) Kaskazini mwa Kenya na Mashariki mwa nchi ya Rwanda. Hata hivyo Ugonjwa huo haupo hapa nchini. Kutokana na kuwepo kwa ugonjwa huu katika nchi jirani, Wizara inatoa   maelekezo   yafuatayo kwa Halmashauri zote nchini (Idara za Mifugo, Afya na Elimu) na mikoa yote kuzingatia yafuatayo ili kuchukua tahadhari zote zinazotakiwa ili ugonjwa huu usiweze kuingia nchini. (a)       Halmashauri zianze kutoa taarifa n...

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI YA KUTEMBELEA WAFUGAJI WA SAMAKI NA WAZALISHAJI WA CHAKULA CHA SAMAKI KATIKA MKOA WA PWANI.

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega lifanya Ziara yake katika Wilaya za Kibaha na Bagamoyo ya kuwatembelea wadau wa Ukuzaji viumbe kwenye maji ambapo walipata fursa ya kueleza shughuli wanazozifanya pamoja na changmoto wanazozikabili, hivyo lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli zilizopo katika Sekta ya Uvuvi. Naibu Waziri alianza ziara yake kwa kuwatembelea na kuongea na wamiliki pamoja na wafanyakazi wa Shamba la Ufugaji wa Samaki la Ruvu Wilaya ya Kibaha Kata ya Mbwawa ambapo alipata fursa a kusikiliza shughuli zao na changamoto zinazowakabili ikiwemo upatikanaji wa Chakula cha samaki. Meneja wa Shamba la Ruvu Bw. Kumbo alisema katika taarifa yake tatizo kubwa linalowakabili ni upatikanaji wa chakula cha kuku pamoja na suala la umeme." "Tunashindwa kumudu gharama za umeme ni kubwa sana kwa mwezi mmoja gharama yake ni milioni 3, vilevile katika chakula cha samaki tunalazimika kuagiza nje ya nchi kwakuwa chakula cha hapa hakina kiwango kinachotakiwa ...