Nav bar

Jumatatu, 16 Oktoba 2017

SERIKALI KUWATOA SADAKA WATENDAJI WATAKAOZEMBEA UVAMIZI MIFUGO TOKA NCHI JIRANI YA KENYA-MPINASERIKALI KUWATOA SADAKA WATENDAJI WATAKAOZEMBEA UVAMIZIWA
MIFUGO TOKA NCHI JIRANI YA KENYA - MPINA

Serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi
wa Mifugo hususani ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.

Hayo yamebainishwa Wilayani Mwanga na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Luhaga Mpina alipozindua rasmi oparesheni maalum ya uvamizi na utambuzi wa
Mifugo hiyo tokea angani.

Mpina alisema kuwa uvamizi wa Mifugo hiyo tokea nchi jirani ya Kenya inaleta
changamoto kubwa ya malisho ya mifugo ya ndani ya nchi inayopelekea migogoro
ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji na husababisha mmomonyoko wa
udongo na uharibifu wa mazingira.

Baada ya kupokea taarifa ya timu ya wataalam iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa
Wizara Mifugo na Uvuvi (Sekta ya mifugo) Dkt Maria Mashingo, iliyofanya oparesheni hiyo maalum kwa kutumia ndege ya shirika la taifa la hifadhi ya wanyamapori, (TANAPA) taarifa
hiyo iliyobaini kuwepo kwa makundi makubwa ya ng’ombe waliokuwa wakihama
kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuwepo kwa idadi kubwa ya Maboma,

 ''Haiwezekani ng’ombe wanaingia kwa makundi makubwa hivi nchini na
watendaji wa serikali wapo, lazima kutakuwa na shida katika utendaji, Oparesheni
hii itakuwa ni ya mwisho, kwa ng’ombe watakaoingia tena watendaji watatolewa
sadaka.” Alibainisha Mpina.

“Yawezekana ng’ombe wote 4000 ambao inasemekana walitoroshwa hapo awali
wapo, hivyo Oparesheni ianze rasmi tuwakamate ng’ombe wote, tuheshimu sana
sheria, na nchi jirani tushirikiane katika mambo tuliyokubaliana kisheria na lolote
litakalotokea katika suala hili la uvamizi wa Mifugo sheria itachukua mkondo wake
na tusilaumiane” Alisisitiza Mpina.

Awali wataalam waliokuwepo katika oparesheni hiyo maalum waliezeza kuwa
mifugo mingi iliyoonekana kutokea angani ilikuwa zaidi katika maeneo ya malisho
na maji ya vijiji vya  kiti cha Mungu,njiapanda,kirya na kitongoi cha Mangulai.
Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushirikiana na kamati ya
ulinzi na usalama ya Wilya ya Mwanga imeingia kazini tayari kwa kuanza
oparesheni hiyo maalum.
Katika picha kikosi kazi maalum cha oparesheni ya angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga inayotokea katika nchi jirani ya Kenya , mbele ni rubani wa ndege hiyo maalum ya TANAPA Bw. Mark Athumani akiongoza ujumbe huo kupanda ndege katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na kikosi kazi maalum kikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Maria Mashingo na Rubani wa ndege hiyo  maalum ya TANAPA Bw. Mark Athumani walipokuwa wakijiandaa kwenda kwenye oparesheni maalum ya angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika wilaya ya Mwanga wanaotokea katika Nchi jirani ya Kenya.


Waziri Mpina akimpungia mkono Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvivi Dkt Maria Mashingo akiwa na baadhi ya wajumbe wakiingia  kupanda ndege maalum kuanza oparesheni ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga wakitokea Kenya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni