Nav bar

Jumatano, 18 Oktoba 2017

NG'OMBE WALIOINGIZWA KATIKA WILAYA YA MWANGA KUTOKA NCHINI KENYA KINYUME NA SHERIA WAPIGWE MNADA-MPINA


NA MWANDISHI MAALUM -MWANGA

Ikiwa ni siku ya nne baada ya kupewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Luhaga Mpina amefanya ziara ya dharula katika Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro jana, na kuagiza uongozi wa Mkoa huo kupitia mwanasheria wa Serikali wa mkoa, ndani ya siku saba kuzipiga mnada ng’ombe zote zilizoingizwa katika kijiji cha Kyerwa kinyume na sheria na taratibu za nchi.

Mpina ameagiza Idadi ya Ng’ombe hao  1325 kupigwa mnada katika zoezi ambalo litasimamiwa na mwanasheria wa serikali, na kusema kuwa vyombo vya dola viendee kuhakikisha kuwa hakuna ng’ombe atakayepita wala kutoroshwa katika hali yoyote ile.

Aidha Mpina amevitaka vyombo vya dola kuendelea kuwasaka ng’ombe zaidi ya 4000 wanaosadikiwa kutoroshwa na kuwakama pamoja na kuchukua hatua stahiki, na amemtaka mhifadhi mkuu (TANAPA) asaidie kutoa vifaa ikiwa ni pamoja na helicopter na drown ili kuweza kusaidia oparesheni za kusaka mifugo iliyotoroshwa na mingine inayoendelea kuingia kinyemela nchini.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira, alieleza kuwa uvamizi huo wa Mifugo unasababisha tishio la kuambukizwa  kwa magonjwa kwa mifuko ambayo mkoa inayo pamoja na uharibifu wa mazingira hali inayopelekea mkoa kushindwa kufikia malengo ya kujitengea maeneo ya ufugaji, pamoja na  uhaba mkubwa wa malisho na uhaba wa maziwa ambapo mwanga pekee ina ng’ombe zaidi ya 18,000.

Akiongea katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kutoka Sekta ya Mifugo Dkt Maria Mashingo alisema kwa kuwa ng’ombe hao wanatakiwa kuchukuliwa vipimo ili kujua kama wameathirika na magonjwa ya mifugo kwa na aliafiki wazo la kuteketeza kabisa ng’ombe hao endapo watapatikana na magonjwa yasiyotibika.

Madhara mengine yaliyoelezwa kutokana na uvamizi wa mifugo hiyo ni pamoja na uharibifu wa vyanzo vya maji, misitu na ongozeko la migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

 


Kulia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kiliminjaro Mhe. Anna Mghwira  kushoto, alipokuwa akimuelezea kuhusu uingizwaji haramu wa mifugo aina ya ng’ombe, wanaosadikiwa kutoka nchi jirani ya Kenya unaofanywa na wafugaji wa nchi hiyo.


Katika Picha Waziri Mpina akiwa katika kikao na uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro alipofanya ziara ya Dharula, baada kuwepo kwa uvamizi wa mifugo kutoka Kenya.


Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kushoto na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Mifugo Dkt Maria Mashingo walipokuwa katika kikao na uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro.


Katika picha, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na Baadhi wa wafugaji na Viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro hawapo katika Picha, alipofanya ziara ya dharula katika kijiji cha Kyara wilayani Mwanga ambapo umetokea uingizwaji wa mifugo kinyume cha sheria na wafugaji wanaosadikika kutoka nchi jirani ya Kenya.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni