Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2026

DKT. BASHIRU AFANYA MAZUNGUMZO NA FAO KUENDELEZA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Nchini Tanzania Dkt. Nyabenyi Tipo  na kufanya mazungumzo yanayolenga kuendeleza ushirikiano  katika kukuza na kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Januari 29, 2026 katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi  zilizopo Kambarage Tower Jijini Dodoma ambapo Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini Tanzania Dkt. Tipo ametumia nafasi hiyo, pia kujitambulisha na kumpongeza Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kukurwa kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Akizungumza Katika kikao hicho Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema serikali ya awamu ya sita imetoa kipaumbele kwenye bajeti kwa sekta za uzalishaji ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi, hivyo juhudi zinazofanywa na FAO katika  sekta za  uzalishaji ni  ishara ya kuimarisha uchumi wa wananchi, na kum...

SERIKALI YAELEZA MKAKATI WA WA KUENDELEZA MINADA YA MIFUGO

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imeeleza mkakati wa Serikali wa kuendeleza Mnada wa Mifugo wa Magena uliopo mpakani, kwa lengo la kukuza biashara ya mifugo na kurahisisha usafirishaji wa mifugo kwenda katika nchi jirani.  Hayo yamesemwa Leo Januari 29,2026 Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Kamani, wakati akijibu la swali la mbunge wa Tarime Mjini Mhe. Esther Matiko,aliyetaka kujua  mkakati wa Serikali wa kuendeleza mnada wa Mifugo wa Magema, amesema Mnada wa Magena. “Katika jitihada za kuendeleza mnada huo, serikali imeendelea kuboresha miundombinu muhimu ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022, kiasi cha shilingi milioni 175.65 kilitengwa na kutumika kujenga mazizi, kipakilio, birika la maji pamoja na vyoo, na miundombinu hiyo imekamilika.”Mhe. Kamani. Aidha, amesema kuwa pamoja na uwepo wa miundombinu hiyo, Mnada wa Magena bado haufanyi vizuri kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo utoroshaji wa mifugo kwenda nchi jirani unaofanywa na baad...

KAMANI ATAJA MIKAKATI YA SERIKALI KUONGEZA MAENEO YA MALISHO

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza kutekeleza mkakati wa miaka mitano wa kuongeza maeneo kwa ajili ya shughuli za ufugaji kwa kutenga hekta milioni 2.51, ikiwa ni sehemu ya kuongeza maeneo yaliyopimwa na kutengwa kwa shughuli za ufugaji kutoka hekta milioni 3.49 hadi hekta milioni sita kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) ya mwaka 2025- 2030 na hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kufungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Novemba 14, 2025. Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani  leo Januari 28, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Yannick Ikae Ndoyinyo lililohoji serikali inampango gani wa kuongeza maeneo ya malisho kutoka hekta milioni Tatu hadi hekta milioni sita kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inavyosema?. “Mhe. Spika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wiz...

DTK. BASHIRU AITAKA TADB KUONGEZA WIGO WA MIKOPO SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa( Mb.) amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TABD) na kufanya mazungumzo  na yanayolenga kuendeleza ushirikiano kati ya wizara na benki hiyo  na kuitaka kuendeleza miradi ya sekta za mifugo na uvuvi. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 27 Januari 2026 katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyopo Kambarage Tower Jijini Dodoma, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TADB alifika kujitambulisha kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara hiyo na Benki ya TADB katika kuendeleza sekta za Mifugo na Uvuvi. Katika Mazungumzo hayo Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameipongeza Benki ya TADB kwa jinsi inavyoshirikiana na wizara na kuiagiza  kupanua wigo wa kuwasaidia wafugaji wadogo kupata mikopo nafuu ili waweze  kuendeleza miradi yao, pamoja na kuongeza ushiriki wa Taasisi za kifedha kupitia TADB katika kutoa mikopo kwenye Sekta ya Mifugo na Uvuvi. Kwa upande wa Mkur...

VCT YASAJILI WATAALAM WA MIFUGO 293 WENYE SIFA STAHIKI

Picha
Na. Stanley Brayton, WMUV ◾ Vituo 130 vya Huduma za Afya ya Wanyama vysajiliwa. Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) limekamilisha mapitio na kusajili Wataalam wa Wanyama wenye sifa stahiki, pamoja na kusajili Vituo mbalimbali vya kutoa Huduma za Afya ya Wanyama, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Sheria ya Veterinari SURA 319. Akizungumza katika Kikao cha 62 cha Baraza cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza hilo kwa Robo ya pili ya mwaka wa 2025/2026, leo Januari 27, 2026 Dodoma, Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), Prof. Lughano Kusiluka amesema Baraza limepitia na kuridhia kuwapa usajili watoa Huduma za Afya ya Wanyama 293 na Vituo 130 vya utoaji Huduma za Afya ya Wanyama. “usajili huu umefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Veterinari SURA 319, kwa kuangalia vigezo mbalimbali stahiki.” amesema Prof. Kusiluka Aidha, Prof. Kusiluka amewataka Wataalam hao na Vituo hivyo kutoa Huduma hizo kwa uweledi na utaalam kwa wafugaji na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za...

MHE. KAMANI AINADI MAMLAKA YA UVUVI BUNGENI

Picha
◼️Agusia pia uwekezaji kwenye Viwanda vya nyama Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani amelieleza Bunge kuwa katika kukabiliana na changamoto ya Uvuvi usiofuata sheria Serikali kupitia Wizara yake ipo kwenye hatua za mwisho za kuanzisha mamlaka ya Uvuvi itakayofanikisha kudhibiti changamoto hiyo kwenye maeneo yote ya Uvuvi nchini. Mhe. Kamani amesema Januari 27,2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge mbalimbali waliotaka kufahamu hatua ambazo Serikali imechukua katika kudhibiti vitendo vya Uvuvi usiofuta Sheria ambapo amesema kuwa hatua hiyo itarahisisha utekelezaji wa Mpango kabambe wa sekta ya Uvuvi wa mwaka 2021-2037 wenye kipumbele cha kuanzisha, kufufua, kuendeleza na kuimarisha viwanda vya kuchakata mazao ya Uvuvi nchini. “Mhe. Spika ili kuhakikisha viwanda vyetu vinafanya kazi kulingana na matarajio ya Serikali, Wizara ipo katika hatua za maamuzi kulingana na taratibu za Serikali  kuanzisha mamlaka ya Uvuvi kwa lengo la Usimamizi wa rasilima...

DKT. BASHIRU AZIAGIZA LITA, TARILI KUFANYA MAGEUZI SEKTA YA MIFUGO

Picha
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ameitaka Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kutumia mafunzo na tafiti za mifugo za kisasa  kuwanufaisha wafugaji nchini. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ametoa agizo hilo leo Januari 24, 2026 wakati wa ziara yake kwenye taasisi hizo zilizopo Mabuki mkoani Mwanza, ambapo amesema tafiti na mafunzo  ya mifugo yanayoendana na wakati yatumike kuwabadilisha wafugaji kufuga kisasa. “Utafiti wetu mzuri, mafunzo yetu mazuri vitumike kwenda kubadilisha wafugaji, sisi tuwachague wale ambao wameshabadilika na wamewekeza , tuwape utaalam zaidi ili watumike kama wasambazaji wa teknolojia” alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru. Aidha, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru aliitaka LITA kufanya ufuatiliaji wa utaalam unaotolewa kwa wafugaji kutokana na mafunzo yanayotolewa na Wakala huo huku TALIRI ikiagizwa kufuatilia matumizi ya tafiti kutoka kwa wadau wa sekta ya mifugo. Katika hatua nyingine ali...

TAWFA YAJIVUNIA MAFANIKIO WALIYOYAFIKIA, WAISHUKURU SERIKALI

Picha
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wanaojishughulisha na Uvuvi Tanzania (TAWFA), Bi. Beatrice Mmbaga amekutana na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agness Meena, Jijini Dodoma Januari 22, 2026 kwa lengo la kuishukuru serikali na kueleza mafanikio waliyoyapata  tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019.  Mwenyekiti huyo  wa TAWFA, Bi. Mmbaga akiwasilisha taarifa yake ya mafanikio alisema  kuwa TAWFA imefanikiwa kuanzisha kanda mbalimbali ikiwemo  Kanda ya Maji ya Bahari na Pwani, Kanda ya Ziwa Tanganyika, Kanda ya Ziwa Victoria pamoja , Kanda ya Ziwa Nyasa na Maji Madogo huku akifafanua kuwa hatua hiyo imeongeza ushiriki wa wanawake, upatikanaji wa mitaji elimu na vitendea kazi.  “Zaidi ya wanawake 2000 wa TAWFA wamefaidika na VICOBA kwa kupata mikopo yenye riba nafuu yenye thamani ya Tshs. zaidi ya 160,000,000, huku TAWFA ikiendelea  kuimarika kwa kitambulika kikanda na Kimataifa ambapo sasa ni mwanachama wa World FisherFolks na African Women FishWorker...

SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI KUONGOZWA KISAYANSI

Picha
Na. Edward Kondela Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema serikali itazingatia masuala ya kitaalamu, ushauri wa kisayansi na tafiti katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amebainisha hayo leo (22.01.2026), alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, ili kuweka pamoja makubaliano ya kushirikiana kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na SUA. Akizungumza na baadhi ya wanachuo, wakati akijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa chuoni hapo, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza kuzingatia masuala ya kitaalamu, ushauri wa kisayansi na tafiti katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi. “Wizara imepewa maelekezo ya Mhe. Rais pamoja na Dira ya Maendeleo ya miaka 25 inatuelekeza kutoka kufuga kienyeji na kufuga kisasa pamoja na kufuga kwa tija na ufanisi.” Amefafanua Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Aidha, ameongeza kuwa SUA ni moja ya v...

SEMINA YA MAFUNZO ELEKEZI KUHUSU SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI YAKAMILIKA

Picha
 Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Taasisi zilizopo chini yake imehitimisha Semina ya Mafunzo Elekezi iliyotolewa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kuhusu shughuli zinazo ratibiwa na kusimamiwa na Wizara hiyo. Akizungumza kwenye tamati ya semina, Mwenyekiti  wa Kamati hiyo Mhe. Deudatus Mwanyika aliwapongeza viongozi pamoja na wataalam wa wizara hiyo kwa uwasilishaji mzuri wa semina hiyo ya siku 2 iliyoanza Januari 19, 2026 na kuhitimishwa leo Januari 20, 2026 Bungeni Jijini Dodoma. Aidha Mhe. Mwanyika amesisitiza wizara kuendelea kuboresha matumizi ya teknolojia za kisasa za kitafiti pamoja na mafunzo yanayoendana na teknolojia hiyo kwa watumishi na wataalamu wa sekta zote ili kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na uvuvi. Akitolea ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa kamati hiyo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema Wizara yake inaendelea kuimarisha na kuboresha huduma zinazot...

BUNGE LAPIGWA MSASA KUHUSU SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wamepewa semina  kuhusu Majukumu mbali mbali yanayofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Taasisi zake. Semina hiyo ya siku 2 imeanza leo Januari 19, 2026 Bungeni Jijini Dodoma ambapo mara baada ya kupewa semina hiyo wabunge hao kupitia kwa Mwenyekiti  wa Kamati hiyo Mhe. Deudatus Mwanyika walitoa maelekezo mbalimbali ikiwemo kuharakisha mchakato wa kuunda Mamlaka ya uvuvi nchini ili kusaidia usimamizi wa rasilimali za uvuvi na kuongeza tija ya kiuchumi na usalama wa chakula kupitia uzalishaji wa malisho ya mifugo. “Pamoja na Jitihada hizo, lakini tunaomba huu mchakato wa kuunda mamlaka ya uvuvi uharakishwe kwa sababu usimamizi wa uvuvi bado unachangamoto, vilevile suala la malisho liangalieni “ alisema Mhe. Mwanyika. Akitolea ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa kamati hiyo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa...

SERIKALI, IFAD KUENDELEZA MIRADI YA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI.

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ambapo wamejadili kuhusu miradi inayotekelezwa kuendeleza sekta ya mifugo na uvuvi. Akizungumza katika Kikao hicho kilichofanyika leo Januari 16, 2026, Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameonesha kufurahishwa na ujio wa ujumbe huo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa IFAD nchini. Amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuimarisha mazingira kuwa rafiki ili kuruhusu wawekezaji na sekta binafsi kushiriki katika kusukuma maendeleo ya wananchi. Ujumbe huo wa IFAD  umeongozwa na Mkurugenzi wa Nchi na Mwakilishi wake nchini Tanzania Bw. Seth Meng pamoja na Mratibu wa Mpango wa Nchi wa IFAD Bi. Jacqueline Machangu. Majadiliano hayo yalijikita kujadili mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) na Mradi wa Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayotekelezwa kati ya se...