Nav bar

Jumatatu, 17 Machi 2025

 SERIKALI YATAMBULISHA MRADI MPYA WA KIMAGEUZI KATIKA TASNIA YA MAZIWA 

Na. Stanley Brayton

Serikali imeendelea kufanya juhudi za kuimarisha na kuweka mikakati  bora ya kukuza Tasnia ya Maziwa kwa kutambulisha Mradi mpya wa Kimageuzi  wa Tasnia hiyo.

Akizungumza katika  Warsha hiyo ya  kutambulisha  Mradi wa Kimageuzi wa Tasnia ya Maziwa iliyofanyika leo Machi 17, 2025 mkoani Dodoma katika Ukumbi  wa Hoteli ya Rafiki, Katibu Mkuu Wizara  ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, amesema Mradi huu utagharimu kiasi cha Dola 174.36 za Kimarekani na ni muhimu sana kwa watanzania wengi.

"tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kuwepo kwa Mradi huu ambao utasaidia kunyanyua uchumi wa Watanzania na nchi kiujumla" amesema Prof. Shemdoe 

Aidha, Prof. Shemdoe ameelekeza kuwa Mradi huo uzingatie thamani ya fedha, muda pamoja na matokeo  chanya yanayolenga kuwanufaisha vijana, wakina mama pamoja na makundi maalum 

Vilevile, Prof. Shemdoe ameeleza kuwa Mradi huo ni Muunganiko wa Tanzania Bara na Visiwani unaotarajiwa kufika katika Mikoa 10 na Wilaya 28.

Prof. Shemdoe amewashukuru wadau wa maendeleo pamoja na wadhamini ambao ni IFAD, OPEC Fund, AFD, Irish League of Credit Union's Foundation (ILCUF), HEIFER, International Tanzania (HI), Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) na FAO.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo - Zanzibar, Ndg. Ali Khamis Juma, amesema Mradi huo unategemewa kuinua kipato na maisha ya Mtanzania hususani kwa wafugaji kwani Seerikali imejipanga kushirikiana na wafugaji wadogo na kuwasaidia kukua katika tasnia ya Maziwa.

Pia, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Stephen Michael, amesema Maziwa yanachangia kwa asilimia kubwa pato la Taifa, japo kunahitajika kuhakikisha upatikanaji wa Maziwa unatakiwa kuwekewa Mazingira mazuri ikiwemo kuboresha Malisho na upatikanaji wa maji, Huduma za Ugani, Tafiti, mafunzo na Masoko kwa ajili ya wafugaji.

Naye, Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. George Msalya amesema Tasnia ya Maziwa ina changamoto nyingi zikiwemo Uzalishaji mdogo wa Maziwa, Masoko na ukusanyaji wa Maziwa ambao unachangiwa sana na mabadiriko ya hali ya hewa, kwa hiyo Mradi huu utaenda fanya Mageuzi makubwa kitasnia.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, akihutubia wadau wa Tasnia ya Maziwa, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Ndg. Ali Khamis Juma, akielezea hali ya Tasnia ya Maziwa Zanzibar, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo  na Uvuvi (Mifugo), Ndg. Abdul Mhinte, akizungumza na wadau wa Tasnia ya Maziwa, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo  na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede, akizungumza na wadau wa Tasnia ya Maziwa, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Stephen Michael, akitoa utangulizi, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma
Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo Tanzania (IFAD),Bw. Sakphouseth Meng, akizungumza na wadau wa Tasnia ya Maziwa, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma
Mkurugenzi wa AFD Tanzania, Bi. Celine Robert, akizungumza na wadau wa Tasnia ya Maziwa, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa  la HEIFER Tanzania, Bw. Mark Tsoxo, akizungumza na wadau wa Tasnia ya Maziwa, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma
Mratibu na Kiongozi wa Kiufundi wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa, Ndg. Lazaro Kapella, akitambulisha Mradi huo kwa wadau wa Tasnia ya Maziwa, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli, Machi 17, 2025, Dodoma

Picha ni baadhi ya wadau wa Tasnia ya Maziwa walioshiriki ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli , Machi 17, 2025, Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo  na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (katikati waliokaa), akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Tasnia ya Maziwa, ni katika Warsha ya kutambulisha Mradi wa Mageuzi wa Tasnia ya Maziwa  na Mabadiriko ya Tabia ya nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Rafiki Hoteli , Machi 17, 2025, Dodoma.