Nav bar

Alhamisi, 14 Septemba 2023

ULEGA AALIKA WAWEKEZAJI KUUNGA MKONO BBT

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewaomba Wadau na Wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza katika programu ya BBT ili kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuinua wanawake na vijana kupitia sekta za mifugo na uvuvi.

Waziri Ulega alitoa wito huo wakati wa hafla fupi ya kujenga uhusiano na ushirikiano baina ya Wadau na Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi iliyoandaliwa na Shirika la Heifer International ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF).

Wakati akiongea na wadau na wawekezaji mbalimbali walioshiriki hafla hiyo, Mhe. Ulega alisema kuwa  BBT ni programu ya kielelezo ya Mhe. Rais, Dkt Samia na mpaka sasa Serikali imeshawekeza kiasi cha shilingi bilioni 20.3, lakini ili programu hiyo iweze kufanikiwa na kuwa endelevu inahitaji kuungwa mkono na wadau kwa namna mbalimbali ikiwemo fedha na tekinolojia.

"BBT ni programu ya kielelezo ya Rais, Dkt. Samia na wadau mbalimbali wakiwemo Wadau wa maendeleo na sekta Binafsi wameonesha nia ya kuiunga mkono wakiwemo heifer international, nitumie nafasi hii kuwaomba Wadau wa maendeleo na sekta Binafsi mjitokeze kwa wingi katika kuunga mkono jitihada hizi za Mhe. Rais za kuwainua wanawake na vijana," alisema

Aidha, alitumia nafasi hiyo pia kulishukuru Shirika la Heifer International kwa kuendelea kuwa miongoni mwa wadau muhimu katika sekta ya mifugo, huku akiwapongeza kwa mradi wao wa Kopa Ng'ombe, Lipa Maziwa ambao ng'ombe takriban 300, 000 walikopeshwa kwa wafugaji wadogo wa ng'ombe wa maziwa  hapa nchini.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na Wadau na Wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi waliojitokeza wakati wa hafla fupi ya kujenga uhusiano na ushirikiano baina yao iliyoandaliwa na Shirika la Heifer International ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF).

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Heifer International hapa nchini, Mark Tsoxo (katikati) pamoja na mdau mwingine wakati wa hafla fupi ya kujenga uhusiano na ushirikiano baina yao iliyoandaliwa na Shirika la Heifer International ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu, Prof. Riziki Shemdoe (wa pili kutoka kulia) wakiwa na Mkurugenzi wa Heifer International hapa nchini, Mark Tsoxo (wa kwanza kushoto) pamoja na mdau mwingine wakiwa katika hafla fupi ya kujenga uhusiano na ushirikiano baina yao iliyoandaliwa na Shirika la Heifer International ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni