Mshauri Mwelekezi kutoka
Shirika la Chakula na Kilimo Duniani
(FAO) Bw. Monday Ahonsi akieleza lengo la shirika hilo kutoa msaada wa
compyuta kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa ni pamoja na kusaidia kwenye
shughuli za kituo cha huduma kwa wateja kinachotarajiwa kianzishwa wizarani hapo,
Septemba 12,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha
Teknolojia ya habari na Mawasiliano (TEHAMA) Bw. Baltazari Kibola (kulia)
akichangia hoja wakati wa kikao kifupi na wawakilishi kutoka Shirika la Chakula
na Kilimo Duniani (FAO) kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Mifugo na
Uvuvi mtumba jijini Dodoma , Septemba 12, 2023
Kaimu Katibu Mkuu kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (kushoto) akipokea msaada wa
kompyuta zitakazosaidia kwenye kituo cha huduma kwa wateja kinachotarajiwa
kuanzishwa kwenye Wizara hiyo kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).
Bw. Monday Ahonsi (wa pili kutoka kulia)
mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika
mtumba jijini Dodoma, Septemba 12,2023.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (wa nne kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kupokea msaada wa kompyuta kutoka FAO, Septemba 12, 2023 jijini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni