Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 13 Sept 2023, ameshiriki ufunguzi wa mkutano unaoandaa andiko la mradi wa kuongeza uzalishaji wa maziwa huko Kigali nchini Rwanda kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi, na kupunguza gesi joto kwa nchi nne za Africa Mashariki (Kenya, Rwanda, Tanzania, na Uganda)
Aidha, Mkutano huo wa siku tatu unaofanyika nchini humo, Prof.Shemdoe amewaelekeza washiriki kufikiria kuelekeza fedha na utaalam wa mradi huo kwa Upande wa Tanzania katika maeneo sita ambayo ni pamoja na BBT-LIFE, kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake, kuongeza utajiri kwa wadau, kuongeza uzalishaji, kuimarisha mradi wa kopa ng'ombe lipa maziwa na kutilia mkazo suala la "Livestock Guest House".
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 13.09.2023 akifuatilia kwa
makini Mkutano wa uandaaji wa andiko la mradi wa kuongeza uzalishaji wa maziwa
kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza gesi joto kwa nchi za Africa Mashariki.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe (Kushoto) akiteta jambo leo tarehe
13/09/2023, na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na rasilimali za Mifugo wa Rwanda
Dr. Olivia Kamana ambapo pia wamekubaliana kuwa na mpango wa pamoja wa chanjo
ya Mifugo.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe, leo tarehe 13 Sept 2023 akizungumza akiwa
Kigali nchini Rwanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Uandaaji wa
andiko la mradi wa kuongeza Uzalishaji wa Maziwa kwa kuzingatia madiliko ya
tabia nchi na kupunguza gesi joto kwa nchi za Africa Mashariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni