Nav bar

Alhamisi, 20 Julai 2023

WADAU WAKUTANA KUJADILI RASIMU YA KANUNI MPYA YA USAJILI NA UDHIBITI WA VIUATILIFU VYA WANYAMA ZA MWAKA 2023

 

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga akifungua kikao cha Wadau (hawapo pichani) cha kujadili Rasimu ya Kanuni Mpya ya Usajili na Udhibiti wa Viuatilifu vya Wanyama za mwaka 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA uliopo Temeke Jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 04/07/2023.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akitoa ufafanuzi kuhusiana na Rasimu ya kanuni mpya ya Usajili na Udhibiti wa Viuatilifu vya Wanyama za mwaka 2023 kwenye kikao cha wadau wanaohusika na Viuatilifu vya Wanyama (hawapo pichani) tarehe 04/07/2023 katika ukumbi wa TVLA uliopo Temeke Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau wanaohusika na Viuatilifu vya Wanyama siku ya tarehe 04/07/2023 kwenye kikao cha kujadili Rasimu ya Kanuni Mpya ya Usajili na Udhibiti wa Viuatilifu vya Wanyama za mwaka 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA uliopo Temeke Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa TVLA Dkt. Stella Bitanyi.

Matukio mbalimbali katika picha za Wadau wanaohusika na Viuatilifu vya Wanyama wakijadili rasimu ya Kanuni Mpya ya Usajili na Udhibiti wa Viuatilifu vya wanyama za mwaka 2023 katika makundi kwenye kumbi za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA zilizopo Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 04/07/2023







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni