Nav bar

Alhamisi, 20 Julai 2023

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MAONYESHO YA 47 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA

 

Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Ugani(mifugo) Dkt. Angello Mwilawa alipotembelea banda la TAFICO lililopo katika Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika viwanja vya Sabasaba leo tarehe 05.07.2023 na kupata maelezo ya jinsi TAFICO ilivyojipanga kutekeleza miradi yake hasa uvuvi wa Bahari Kuu kutoka kwa Afisa Uvuvi Mkuu Bw.Mgalula Lyoba

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (Mifugo) Kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angello Mwilawa akisaini kitabu cha wageni alipotemblea banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na Wakala siku ya tarehe 05/07/2023 kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (Mifugo) Kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Angello Mwilawa (alievaa kofia) akipata maelezo kuhusiana na matumizi ya sahihi ya chanjo ya Mdondo wa kuku aina ya TEMEVAC kutoka kwa Mtaalam wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Dkt. Richard Mwakapuja alipotemblea banda la TVLA kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na Wakala kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam siku ya tarehe 05/07/2023.

Mtaalam kutoka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Bwana Mashaka S. Kapagalla akitoa elimu kwa wadau wa Uvuvi waliotembelea banda la FETA kujionea mbinu bora za uzalishaji wa vifaranga vya Samaki aina ya Sato na kambale pamoja na ufugaji wa jongoo bahari siku ya tarehe 05/07/2023 kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam





Mtaalam kutoka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Bwana Godfrey Christopher akitoa elimu kwa wadau wa Uvuvi waliotembelea banda la FETA kuhusiana na kilimo cha Mwani (Seaweeds), uchakataji wa mazao ya Mwani pamoja na faida zake kiafya na kiuchumi siku ya tarehe 05/07/2023 kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam

Wadau mbalimbali wa Uvuvi waliojitokeza kwenye banda la Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) lililopo kwenye eneo la Mifugo na Uvuvi kupata elimu kuhusiana na mbinu bora za uzalishaji wa vifaranga vya Samaki aina ya Sato na kambale, ufugaji wa jongoo bahari, kilimo cha Mwani (Seaweeds), uchakataji pamoja na faida zake kiafya na kiuchumi kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam



Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini Dkt. Immaculate Sware Semesi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda la Wizara ya Mifugo Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es salaam,  Julai 05,2023

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angello Mwilawa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) Bw. Hamisi kihimbi,  wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 05,2023

Afisa Uhusiano kutoka Kampuni ya Ranchi za Taifa Tanzania  (NARCO) Bw. Jumanne Mutalemwa, akitoa elimu ya utaratibu wa upatikanaji wa vitalu, na manufaa ya uwepo wa NARCO Tanzania kwa wadau  waliotembelea  banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam,  Julai 05,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi.(TAFIRI) Bi. Julietha Basil Mosille akitoa elimu kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 05,2023

Sehemu ya wadau wakiingia na kutoka kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 05,2023

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni